Sunday, September 21, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

TOFAUTI na wengi walivyotarajia, kocha mkuu wa Simba sc, Mzambia, Patrick Phiri amefanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake kuelekea mchezo wa jioni hii, ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Coastal Union.

Mkenya Raphael Paul Kiongera ameanzia benchi, wakati Mganda Emmanuel Okwi ameanza katika kikosi cha kwanza.

Phiri amewaanzisha Piere Kwizera na Emmanuel Okwi sehemu ya washambuliaji wa kati, wakati Haruna Chanongo anashambulia kutoka winga ya kulia na Ramadhani Singano ‘Messi’ anashambulia kutoka kushoto.

Mkongwe Shaaban Kisiga ‘Malone’ ameanza kama kiungo mchezeshaji, wakati mfungaji bora wa msimu uliopita, Amissi Tambwe ameanza kama kiungo wa ulinzi.

Langoni atasimama kipa mkongwe Ivo Mapunda, wakati kulia anaanza Miraji Adam na kushoto anaanza Mohamed Hussein ‘Tshabalala.

Walinzi wa kati ni Hassan Isihaka na Joseph Owino.

Wachezaji wa akiba ni Hussen Sharif, Nassor Masoud, Said Hamis, Joram Mgeveke, Amri Kiemba, Uhuru Seleman na Rapahel Paul Kiongera.



Kikosi cha Simba hiki hapa:


0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video