Sunday, September 21, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

PAUL Kiongera leo jioni anatarajia kuiongoza Simba dhidi ya Coastal Union katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara itakayopigwa uwanja wa Taifa, Dar es salaam.

Kiongera anayeonekana kufunika jina la mfungaji nyota wa Simba msimu uliopita, Mrundi Amissi Tambwe, anatazamwa kwa jicho la tatu kutokana na kiwango chake alichoonesha kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, septemba 6 mwaka huu na nyinginezo.

Mbali na kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0, Kiongera alionesha soka safi na kukonga nyoyo za mashabiki wa Simba waliofurika kwa wingi uwanjani.

Simba walionekana kubadilika katika mechi hiyo wakicheza soka la chinichini, pasi za uhakika na kupanga mashambulizi mazuri kutokea sehemu ya kiungo.

Ramadhani Singano ‘Messi’, Uhuru Seleman, Shaaban Kisiga, Okwi, Kiongera walionekana kuwa katika ubora wa juu.

Katika mechi nyingine ya kimataifa ya kirafiki, Simba walifungwa bao 1-0 na URA ya Uganda na kutoka suluhu ya bila kufungana na Ndanda fc katika mechi ya mwisho ya kujipima ubavu.
Baada ya mechi hiyo, Simba wamekaa takribani wiki moja visiwani Zanzibar na walirejea jana Dar es salaam tayari kwa mechi ya leo.

Haifahamiki ni kwa kiasi gani kocha Patrick Phiri amefuta makosa yaliyojitokeza katika mechi za mwisho za kirafiki kwasababu hajacheza mechi nyingine, lakini katika mazoezi ya Zanzibar, Simba walionekana kuwa imara.

Katika mazoezi hayo, wachezaji wa Simba walizidi kumuonesha Phiri kuwa wanajua wanachokifanya ingawa msimu uliopita waliangushwa na kocha aliyetimuliwa Zdravko Logarusic.

Phiri amekuwa akiwafundisha vijana wake jinsi ya kujilinda, kupiga pasi za uhakika, kumiliki mpira na kushambulia kwa kasi.

Utamaduni wa soka la Tanzania hususani Simba sc ni mpira wa pasi ‘passing football’ na mashabiki wengi wanapenda hivyo.

Katika mechi dhidi ya Gor Mahia walionesha ladha ya mpira huo uliopotea kwa muda mrefu, ingawa katika mechi ya URA hawakucheza katika kiwango chao.

Leo Simba wanakutana na Coastal Union wakiwa na sura mpya kikosini baada ya kufanya usajili mzuri.

Wachezaji kama Tshabalala, Shaaban Kisiga, Piere Kwizera, Kiongera, Emmanuel Okwi, Abdi Banda na wengineo ambao hawakuwepo msimu uliopita wanaweza kuanza.

Coastal Union imekuwa katika mabadiliko makubwa kuanzia uongozi, wachezaji, na wadhamini.

Msimu uliopita walikuwa wanadhaminiwa na Binslum, lakini walivunja ‘ndoa’ hiyo na sasa wanaendelea na maisha mengine chini ya wadhamini wengine.

Waliweka kambi ya mwezi mmoja kisiwani Pemba na wamecheza mechi nyingi za kirafiki kwa malengo ya kujiimarisha.

Matundo ya maandalizi hayo yanatarajia kuonekana katika mechi ya leo wakiwa na kumbukumbu ya kuwafunga Simba 1-0 katika mechi ya mzunguko wa pili msimu uliopita.

Mashabiki wa Simba wamekuwa na imani na kikosi chao kwa sasa, na kwa vile Mtani wao alifungwa jana 2-0 na Mtibwa Sugar, basi itakuwa furaha kubwa kama wataanza kwa ushindi.

Haitakuwa mechi rahisi hata kidogo kwa Simba licha ya kuwa uwanja wa nyumbani. Coastal Union wana historia ya kufanya vizuri dhidi ya Simba hususani wakiwa uwanja wa nyumbani wa Mkwakwani.

Hii itakuwa mechi ngumu sana, lakini kutokana na namna Simba ilivyojengwa vizuri na Phiri, nathubutu kutoa asilimia 60 za ushindi dhidi ya 40 za Coastal Union.


Yawezekana matokeo yakawa tofauti kama ilivyokuwa kwa Yanga jana, lakini nawapa nafasi kubwa zaidi Simba kushinda, ingawa mechi itakuwa ngumu na tunaweza kushuhudia lolote lile.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video