Friday, September 12, 2014

Mkali wa sarakasi, Paul Kiongera akishangilia bao lake la pili dhidi ya Gor Mahia wikiendi iliyopita

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

PAUL Kiongera ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri kwa sasa katika kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba chini ya kocha Patrick Phiri.

Mkenya huyu alitua katika rada za Simba chini ya mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hans Poppe majira ya kiangazi mwaka huu akitokea nchini Kenya.

Jina lake lilipata umaarufu zaidi baada ya kutokea benchi wikiendi iliyopita na kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 waliopata Simba dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Mechi hii ya kimataifa ya kirafiki ilikuwa ya kwanza kwa Phiri tangu arejee kuinoa Simba na leo hii anacheza mechi ya pili ya kimataifa dhidi ya URA ya Uganda.

Wachezaji wa Simba watapata nafasi ya kuwaonesha mashabiki wao kuwa wamejiandaa vizuri wakati huu wa mapinduzi klabuni hapo.

Kiongera kama ataonesha uwezo mkubwa kwa mara nyingine, basi atawashika zaidi mashabiki wa Simba wenye kiu ya mafanikio.

Watatisha?: Wachezaji wa Simba wakishangilia goli la Singano kwenye mechi dhidi ya Gor Mahia jumamosi iliyopita

Naye Ramadhani Singano ‘Messi’ baada ya kufunga moja dhidi ya Gor Mahia, ataonesha kiwango kile kile au ataongeza? Dakika 90 zitadhihirisha.

Katika mechi dhidi ya Gor Mahia, Simba walicheza vizuri hususani kipindi cha pili ambapo Safu ya kiungo ilishirikiana vizuri na safu ya ushambuliaji.

Wachezaji kama Uhuru Seleman, Shaaban Kisiga, Awadh Juma, Ramadhani Singano, Paul Kiongera walionekana kuelewana zaidi na kuifanya Simba icheze mpira wake uliopotea kwa muda mrefu.

Walijitahidi kuweka mpira chini, pasi za haraka haraka na za uhakika na kupanga mashambulizi vizuri na hatimaye kupata magoli matatu.

Gor Mahia ambao hawakuonekana kipindi cha pili walijitahidi kushambulia, hususani kipindi cha kwanza, lakini kipa Ivo Mapunda na mabeki wake kama Joseph Owino, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ walicheza kwa kiwango cha juu, wakikaba na kuzuia mianya ya wapinzani kumfikia Ivo.

Je, baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Gor Mahia, leo itakuwaje? Dakika 90 zitatoa jibu.

Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema maandalizi kwa ajili ya mechi ya leo yamekamilika, mambo ya usalama yako safi, hivyo ni fursa ya mashabiki kufurika kuitazama timu yao.

Kaburu alisema wameandaa utaratibu mzuri wa kuuza tiketi ambapo zitaanza kuuzwa leo kuanzia saa 4:00 asubuhi katika magari maalumu yaliyoandaliwa sehemu mbalimbali.

Mbali na mechi ya leo, Kaburu aliongeza kuwa Simba wana mwaliko maalumu kutoka Ndanda fc ili washirikiane kuadhimisha siku ya ‘Ndanda fc Day’ kesho jumamosi.

“Tayari tumeandaa utaratibu mzuri, kikosi kizima cha Simba kikiwa na benchi la ufundi, jumamosi asubuhi, wote watakwenda Mtwara kwa usafiri wa Ndege”


“Siku hiyo jioni tutakuwa pamoja na watu wa Ndanda katika siku yao na kucheza mechi moja ya kirafiki ambayo itakuwa ya mwisho kwetu ya maandalizi na jumatatu tutarudi kambini Zanzibar kabla ya kuanza kwa ligi kuu”. Alisema Kaburu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video