Kiungo wa Chelsea , Eden Hazard amesema hataki kuondoka Chelsea
EDEN Hazard amekanusha taarifa za kuondoka Chelsea kwenda Paris Saint-Germain – licha ya miamba hiyo ya soka ya Ufaransa kuendelea kuvutiwa naye.
Nyota huyo aliyeshinda tuzo ya mchezaji kijana ya PFA msimu uliopita kwa muda mrefu alihusishwa kujiunga na kikosi cha Laurent Blanc majira ya kiangazi mwaka huu, lakini Jose Mourinho alisema atasikiliza ofa itayozidi paundi milioni 150 ili kumuachia mchezaji wake.
Licha ya kuanzia soka lake Ligue 1 kabla ya kujiunga na Chelsea kwa paundi milioni 32 mwaka 2012, Hazard alisema hana nia ya kuondoka klabuni hapo kurudi alikotoka.
Kutokana na kiwango chake, The Blues wanatarajia kumzawadia namba 10 huyo mkataba wa miaka mitano ambapo atalipwa mshahara wa paundi laki mbili kwa wiki na anatarajia kutia saini mwezi ujao.
"PSG wapo ulimwengu ule ule kuliko Chelsea," Hazard aliwaambia Canal+ . "Lakini kama wanataka kuwa klabu ya kiwango cha juu wanatakiwa kushinda ligi ya mabingwa. Nimeridhika Chelsea, ni sehemu ambayo nilipenda kuendelea kukua. PSG hawapo kichwani mwangu"
0 comments:
Post a Comment