Jumanne Athuman Nyamlani (kushoto) akiongea na waandishi wa habari kwenye moja ya mikutano yake siku za nyuma
MICHUANO ya Dr Mwaka SPORTS XTRA
NDONDO CUP inatarajia kufunguliwa kesho (septemba 26 mwaka huu) kwa mechi ya
ufunguzi baina ya Friend’s Rangers na Kiluvya United.
Mechi hiyo kali itapigwa uwanja wa Makulumla, Magomeni, Dar es salaam
kuanzia majira ya saa 10:15 jioni.
Mgeni rasmi katika mechi hiyo atakuwa
Mjumbe wa kamati ya Rufaa ya Shirikisho la soka Afrika, CAF na makamu wa Rais wa
zamani wa TFF, Jumanne Athuman Nyamlani.
Michuano hii itakayoendeshwa kwa mfumo
wa kisasa kabisa itashirikisha wachezaji wa mchangani kutoka timu 32.
Mbali na dimba la Makulumla, viwanja
vingine vitakavyotumika katika mashindano hayo ni Kinesi (Shekilango),
Benjamini Mkapa (Ilala) na Mizinga (Kigamboni).
Mdhamini
Mkuu wa michuano ya Dr Mwaka Sports Extra Ndondo Cup ,Dr Juma Mwaka
akifafanua jambo mbele ya wanahabari kuhusiana na michuano hiyo inayotarajiwa
kuanza kutimua vumbi kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni
jijini Dar es Salaam.
Timu 32 zitakazoshiriki zimepangwa
katika makundi nane yenye timu nne.
Kundi A: Boom fc, Beira Hotspurs,
Tabata fc na Tuamoyo
Kund B: Sifa Politani, Vijana Ilala,
Kijichi, Micco Villa
Kundi C: Friend’s Rangers, Temeke
Market, Kiluvya United na Muheza fc
Kundi D: Ukonga United, Sinza Stars,
Congo Shooting na Snow White
Kundi E: Zakhem, Black Six, TP Same na
Makumba
Kundi F: Villa Squad, Scud fc, Nyota
Afrika na Burudani fc
Kundi H: Stakishari fc, Abajalo,
Shelaton na Kimara United
Kundi G: Temeke United, Sifa United,
Forteagle na Segerea fc.
0 comments:
Post a Comment