
Kikosi cha Mtibwa Sugar msimu uliopita
MTIBWA Sugar wamesema kitendo cha Yanga kuifunga
Azam fc 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii jana uwanja wa Taifa si kigezo cha
kuifunga klabu hiyo katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara,
septemba 20 mwaka huu uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Afisa habari wa klabu hiyo, Tobias Kifaru
Ligalambwike amesema Azam hawakuwa katika kiwango chao licha ya kuwa na nyota
wa ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo amewaonya Yanga kuwa ushindi wa jana
uliochagizwa na Jaja si sababu ya kuamini kuwa watafanya vizuri uwanja wa
Jamhuri Mkoani Morogoro.
“Wasibweteke na ushindi huo na wasiseme tutaanza
ligi kwa kasi. Yanga Wampe Maximo miaka mitano ili ajenge timu mpya kwasababu
ana kikosi cha watu wazima.” Alisema Kifaru.
“Yanga waliifunga Azam kwasababu walikuwa
wagonjwa, hawakuwa katika kiwango chao na ndio maana walifungwa mabao hayo na
wangefungwa mengi zaidi.”
“Sikuona kiwango cha Sure Boy, kijana wangu Himid Mao hakuonekana. Yanga
wasijidanganye.”
0 comments:
Post a Comment