Habari njema!, Christian's Benteke anarudi kuongeza nguvu Aston Villa
CHRISTIAN Benteke anakaribia kupona majeruhi yake na anaweza kurudi uwanjani katika mechi dhidi ya Manchester City jumamosi ya wiki hii.
Aston Villa kwa muda mrefu imecheza bila nyota wake huyo tangu mwezi machi mwaka huu kufuatia kupata majeruhi wakati wa mazoezi.
Benteke-ambaye rekodi yake ilikuwa ni kufunga goli kwa kila mechi ya Villa-pia alizikosa fainali za kombe la dunia na nchi yake ya Ubelgiji.
Nyota huyo mwenye miaka 23 ameanza mazoezi na timu ya kwanza na kocha wake Paul Lambert anaamini atarejea kazini wikiendi.
Kocha wa Aston Villa atakuwa na furaha na huduma ya mshambulaiji wake hatari, Benteke
0 comments:
Post a Comment