Gerard Pique akishangilia baada ya kuifungia Barcelona dhidi ya Apoel kwenye mechi ya ligi ya mabingwa barani ulaya wiki iliyopita
DILI la Manchester United kumsajili Gerard Pique linaweza kuwa gumu baada ya nyota wa Hip hop, Shakira kuweka kupinga.
Mpenzi huyo wa beki wa Barcelona hataki kuondoka katika mji wa Katalunya kwenda Manchester.
Pique hana furaha tena Nou Camp kufuatia nyota mpya Jeremy Mathieu kuchukua namba yake.
Pique (kulia) na mpenzi wake Shakira wakiangalia mechi ya mpira wa kikapu ya FIBA Basketball World Cup mjini Barcelona mapema mwezi huu
Pique (katikati) akisaini mkataba kujiunga na Manchester United mwaka 2004, kulia kwake ni kocha Sir Alex Ferguson na David Gill (kushoto)
Ripoti nchini Hispania zinaeleza kuwa Pique yuko mbioni kurudi Old Trafford wakati huu Louis van Gaal anahitaji mabeki baada ya kuanza msimu vibaya.
Lakini Pique alitiwa moyo na maneno ya kocha wa Barca, Luis Enrique aliyotamka wiki iliyopita.
Kiungi huyo wa zamani wa Nou Camp alisema: "Mtazamo wa Pique ni mkubwa, ni mchezaji mzuri, anajituma. Matatizo yake madogo yametatuliwa, yuko tayari kutusaidia".
Lakini Pique hana mawasiliano na United baada ya kuondoka mwaka 2008.
Shakira na Pique wakifanya yao
0 comments:
Post a Comment