Monday, September 15, 2014

KIKOSI cha Simba kimewasili jioni ya leo visiwani Zanzibar na kesho kinaanza programu ya mwisho ya maandalizi ya kujiwinda na ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ amesema Zanzibar ni sehemu tulivu na rafiki kwa Simba, hivyo kocha Patrick Phiri atatulia huko kabla ya kurejea jumamosi kujiandaa na mchezo wa jumapili (septemba 21 mwaka huu) uwanja wa Taifa, Dar es salaam dhidi ya Coastal Union.

Ijumaa ya wiki iliyopita, Simba walifungwa 1-0 na URA ya Uganda katika mechi ya kimataifa ya kirafiki uwanja wa Taifa na jumamosi walikuwa na mechi na Ndanda fc uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya  mwisho kwa kocha Phiri  kupima uwezo wa kikosi chake ilimalizika kwa suluhu pacha ya bila kufungana.


Kabla ya mechi hiyo, septemba 6 mwaka huu,Simba walishinda mabao 3-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki tangu kocha Phiri arejee msimbazi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video