Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Wakati uongozi wa Simba ukidai kuwa bado una mkataba na beki
Mkenya Donald Mosoti, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeitaka klabu
hiyo kumlipa fidia beki kwa kuwa mkataba wake umevunjwa.
Katibu Mkuu wa Simba, Stephen Ally alikaririwa na baadhi ya vyombo
vya habari nchini jana akisema kuwa Mosoti bado ni mchezaji wao halali kwa vile
mkataba kati yao na mchezaji huyo badi haujavunjwa.
Klabu hiyo kongwe nchini, iliamua kumwacha beki huyo dakika za
mwisho za usajili msimu huu ili kumsajili Emmanuel Okwi aliyevunja mkataba wake
na Yanga huku mwanasheria wa Mosoti, Felix Majani akidai kuwa uamuzi huo
ulifanywa bila kumshirikisha mteja wake.
Mwanasheria huyo anayeishi Ureno amekaririwa na mtandao wa
Futaa.com wa Kenya leo asubuhi akieleza kuwa ilibidi kuvunja mkataba wa Mosoti
na Simba kwanza kabla ya kulifikisha mbele ya FIFA kwa kuwa Simba walikuwa bado
wanadai kwamba Mosoti ni mchezaji wao na walitaka aidha wamuuze au kumtoa kwa
mkopo.
Majani amesema kuwa mteja wake anataka Simba imlipe fidia kwa
kuvunja mkataba wake ilhali alikuwa bado ana muda wa mwaka mmoja na miezi
mitatu kuitimkia klabu hiyo ya Msimbazi. “Kimsingi Mosoti anataka fidia na
ameomba adhabu za kisoka zichukuliwe dhidi ya Simba, kwa kufungiwa kusajili
wachezaji kwa misimu miwili ijayo ya usajili na tayari FIFA imeshauandikia
barua uongozi wa Simba kuukumbusha juu ya kesi hii,” amesema Majani.
Beki wa kushoto Mkenya John Njoroge alikumbana na tatizo kama la
Mosoti dhidi ya Yanga 2011 sought baada ya klabu hiyo ya Jangwani kuvunja mkataba bila kumshirikisha na
baadaye mchezaji huyo alinufaika kwa kupata fidia ya Sh. milioni moja za Kenya,
shukrani kwa maamuzi ya FIFA.
Chanzo:shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment