Kipre Tchetche kwenye moja ya mechi za Azam fc msimu uliopita
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
SAFU ya ushambuliaji ya Azam fc imemtisha beki na
kiungo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Ally Mayay Tembele kuelekea mechi ya
Ngao ya Jamii inayopigwa jioni ya leo majira ya saa 10:00 katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam baina ya mabingwa wa ligi kuu msimu uliopita Azam fc
na washindi wa pili Yanga sc.
Mayay ameiambia MPENJA BLOG mchana huu kuwa safu
hiyo ya ushambuliaji inayoundwa na Mrundi Didier Kavumbagu, Muivory Coast Kipre
Herman Tchetche na Mhaiti Leonel Saint Prexu itampa wakati mgumu kocha mkuu wa
Yanga, Mbrazil, Marcio Maximo.
“Mimi nakwenda kuona nidhamu ya kiufundi kwa
upande wa Yanga, kwasababu Azam ukiangalia kwenye karatasi, safu yao ya
ushambuliaji nafikiri ni nzuri kuliko Yanga, lakini ukiangalia kwenye
makaratasi.” Alisema Mayay.
“Ukiangalia mtu kama Kipre Herman Tchetche, uwepo
wa Mhaiti Leonel Saint Prexu pamoja na Didier Kabumbagu ni hatari sana. Hawa ni
washambuliaji watatu wanaoweza kufanya lolote na wakati wowote. Hata kama mwalimua
(Omog) atawapanga wote au wawili, bado safu yao ni nzuri ukilinganisha na Yanga”.
“Mtu kama Kavumbagu wakati anahama Yanga ndio
kwanza alikuwa ameanza kuwika, kwahiyo nafikiria namna Maximo atavyoweza kuzuia
hiyo safu ya ushambuliaji. Njia pekee ya kuzuia ni kukata mipira yote kutokea
safu ya kiungo ya Azam fc”.
Mayay ambaye kwa sasa ni kocha na mchambuzi wa
soka aliongeza kuwa vipaji binafsi kutoka timu zote pia vinaweza kuamua
matokeo.
“Lakini mechi kama hii wakati fulani, uwezo
binafsi wa wachezaji unaweza kuamua matokeo. Kila timu inaweza kufuata
maelekezo ya walimu kwa asilimia 75 au 80, lakini zinazobaki uwezo binafsi
ukatumika.
“Kwa Yanga kuna mchezaji kama Mrisho Khalfan
Ngassa, lakini kwa upande wa Azam fc kuna wachezaji vijana, kama beki wa
kushoto Gadiel Michael ambaye amekuwa ikiipandisha timu na kutengeneza nafasi”.
0 comments:
Post a Comment