Thursday, September 25, 2014

 Na Baraka Jamali, Mtwara

 Mashabiki wapatao 250 wa Ndanda fc ya Mkoani Mtwara wanaondoka  kesho  saa mbili usiku kuelekea mkoani Morogoro, kwenda kuiunga mkono timu yao  itakayoshuka dimbani jumamosi kumenyana na wenyeji wao Mtibwa Sugar katika uwanja wa jamhuri.

 Mashabiki hao wakiongozwa na mwenyekiti wa kundi hilo Salumu Mabomba wamehamasika na kuwa na imani na timu yao baada ya kupata ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi ya Stand United mwishoni mwa wiki iliyopita. 

 Mashabaki hao ambao wamepania kuwaziba midomo wakata miwa baada kushinda 2-0 katika mchezo wao wa awali dhidi ya Yanga uwanja wa Jamhuri na wameona ni lazima kuwapa morari wachezeji ili waweze kucheza kwa bidii na kuondoka na pointi tatu.

 Kila inapofika mwishoni mwa wiki, mashabiki  wa Ndanda fc iliyopanda daraja msimu huu wamekuwa wakikutana kupanga mikakati na kila mwanachama hutoa mchango wa sh 3000  kwa ajili ya nauli ya kusafiri na timu hiyo kila inapokwenda kucheza nje ya uwanja wao wa nyumbani wa Nangwanda.

 Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa kundi  hilo maarufu kama Ndanda fc kwa roho safi,  Salumu Mabomba, amesema maandalizi ya kuelekea mkoani Morogoro yamekamilika na watu 250 tayari wana uhakika wa kwenda. 

“Tunaondoka  saa mbili usiku kesho ijumaa kuelekea Morogoro kwenda kuipa nguvu timu yetu ya Ndanda na tunataka kuwaonesha watanzania kwamba hatuna masihara katika hili na tunaipenda timu yetu na hatuwezi kuiangusha hata siku moja.  Mtibwa wajiandae na kichapo tu na Vijana wana hamasa kubwa , magari madogo sita yatabeba watu 50, mabasi makubwa manne yatabeba watu 200,”  alisema Mabomba.



Alisema kuwa baadhi ya wadau wamejitokeza na kuwapatia nguvu kwa swala la usafiri  kwa kuwapunguzia bei, hivyo wamewashukuru waendelee kuwa na moyo kama huo na wale ambao wako tayari kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri wanaombwa kujitokeza hata kwa kitu chochote kwa mashabiki hao ambao wameamua kujitoa kwa ajili ya kuiunga mkono timu hiyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video