
Marouane Fellaini akifanya mazoezi katika fukwe huko Ubelgiji
MAROUANE Fellaini alijifua vikali ufukweni huko Ubelgiji wakati wa mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa na lengo lake ni kuwa fiti ili kumvutia kocha wake Louis van Gaal.
Kiungo huyo mwenye 'manywele' mengi alimanusura aondoke Old Trafford mwezi uliopita, lakini majeruhi ya kifundo cha mguu yalimfanya asiwe na thamani.
Klabu ya Napoli chini ya kocha Rafael Benitez ilikuwa tayari kumsajili.
Mazoezi ayafanyayo Fellaini katika fukwe za Sint Anneke yanadhihirisha kuwa anataka kuingia katika mipango ya kocha Van Gaal ambaye havutiwi na Mbelgiji huyu.

Kiungo huyo akijifua kupiga vichwa
0 comments:
Post a Comment