Jack Wilshere alionekana kuushika mpira kwa mkono lakini penalti haikutolewa kwa Manchester City
MANUEL Pellegrini ameponda kiwango cha kocha mkongwe wa England,Mark Clattenburg, akidai kuwa uchezeshaji wake mbaya uliigharimu Manchester City kushindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Arsenal jana uwanja wa Emirates.
Kocha huyo alisema aliwapa magoli mawili Arsenal ambayo kuna madhambi yalifanyika na aliwanyima penalti Man City.
Meneja huyo wa City amekiri kuwa kuna ugumu wa kutetea ubingwa kutokana na upinzani uliopo, lakini alidai kuwa Clattenburg pia aliwahi kuwanyima penalti katika kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Liverpool mwezi aprili mwaka huu na mchezo huo ndio ulionekana kuigharimu City.
Matatizo ya refa na kocha huyo anayeshikilia ubingwa yataendelea kuwa gumzo la msimu kwasababu Clattenburg anapangwa kuchezesha mechi nyingi kubwa.
Madhambi aliyofanya Danny Welbeck kwa nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany pia yamelalamikiwa Manuel Pellegrini
Laurent Koscieln, kwa mujibu wa Manuel Pellegrini, alifanya madhambi kabla ya kumpasia Jack Wilshere aliyefunga bao la kusawazisha
Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini akitoa maelekezo katika mchezo wa jana
0 comments:
Post a Comment