Louis van Gaal alitumia paundi milioni 60 kumsajili winga wa Argentina Angel di Maria kutokea klabu ya Real Madrid
BEKI wa zamani wa Manchester United, Phil Neville anaamini klabu hiyo inahitaji tena paundi milioni 100 za usajili kama wanataka kupambana kusaka ubingwa wa ligi kuu soka nchini England msimu huu.
Msimu uliopita, United walimaliza katika nafasi ya saba na kumsababisha kocha mpya, Louis van Gaal atumie zaidi ya paundi milioni 150 kuwasajili Angel di Maria, Luke Shaw, Ander Herrera, Marcos Rojo, Daley Blind na nyota aliyesainiwa kwa mkopo Radamel Falcao.
United walishindwa kusaini beki wa kati ingawa wameanza msimu kwa kuwatumia Chris Smalling, Phil Jones na Jonny Evans ambao hawaja katika kiwango kizuri, huku beki kinda Tyler Blackett akijitahidi kuimarika.
Van Gaal (katikati) akionekana kuumizwa na kipigo walichoambulia Manchester United dhidi ya Leicester
0 comments:
Post a Comment