LOUIS van Gaal amepata ushindi wa kwanza tangu aanze kuiongoza Manchester United katika michuano ya ligi kuu England kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya QPR.
Mabao ya United katika mechi hiyo iliyopigwa uwanja wa Old Trafford yamefungwa na Juan Mata, Wayne, Ander Herrera na Angel di Maria.
Di Maria aliyeliliwa na Cristiano Ronaldo baada ya kuondoka Real Madrid majira ya kiangazi mwaka huu alifunga bao lake la kuongoza kwa njia ya mpira wa adhabu ndogo.
Herrera alifunga bao la tatu, wakati Wayne Rooney alifunga la tatu na Mhispania, Juan Mata alihitimisha karamu ya mabao.
Radamel Falcao alianzia benchi katika mechi ya leo, wakati Daley Blind na Marcos Rojo walianza katika mechi yao ya kwanza United.
0 comments:
Post a Comment