Na Simon Chimbo
Moja kati ya habari kubwa sana za usajili wa
kiangazi msimu huu nchini Uingereza ni uhamisho wa mshambuliaji mwenye nguvu na
mbio Danny Welbeck kutoka Manchester United kwenda Arsenal kwa ada ya paundi
16m. kijana huyu mwenye miaka 23 pamoja na kubezwa na mashabiki wengi lakini
ana kitu ambacho kwa macho ya kawaida hakikuonekana pale Old Trafford. Ndio
maana sivishangai vilio vya wakongwe wa Manchester United kama Paul Scholes,
David Becham na Rio Ferdinand wakionesha kusikitishwa kwao kwa kuondoka kwa
kijana huyo aliyekulia mjini Manchester tangu akiwa mdogo.
Zifuatazo
ni sababu zinazoweza kumng’arisha Dany Welbeck Arsenal;
1.Kutaka
kuthibitisha uwezo wake
Welbeck kama ambavyo mchezaji yeyote angeweza
fanya, atajituma uwanjani ili kuonesha Manchester United walimuuza kimakosa
huku pia akitaka kuwaondoa shaka mashabiki wa Arsenal kwamba mzee Wenger
hakukosea kumsajili.
2.
Uhakika
wa kucheza kikosi cha kwanza
Kuumia kwa Olivier Giroud kunamfanya Dany awe na
upinzani mdogo na mshambuliaji aliye fiti Yaya Sanogo. Tofauti na ilivyokua
Manchester United, Wayne Rooney na Robin Van Persie walimpa wakati mgumu
Welbeck kupata nafasi kikosi cha kwanza huku usajili wa Radamel Falcao
ungemfanya asipate nafasi kabisa.

3.
Viungo wa Arsenal
Tofauti na Manchester United ambapo hakukua na
viungo wenye uwezo wa kucheza na kutengeneza nafasi kwa washambuliaji wao
kufunga magoli, lakini uwezo wa viungo wazuri kama Jack Wilshere, Mesut Ozil,
Aaron Ramsey, Carzola na wengine, sina shaka Dany atafunga magoli mengi tofauti
na alivyokua Old Trafford.
4.
Matarajio hafifu ya mashabiki wa Arsenal kwa kijana huyo
Presha sio kubwa kwa Welbeck kufanya vizuri kwa
washika mitutu hao wa London kutokana na ukweli kwamba mashabiki wengi wa
gunners hawana uhakika na uwezo wa mshambuliaji huyo raia wa Uingereza na hivyo
Dany anaweza kucheza vizuri kwani mashabiki hawamtarajii makubwa.
5.Uwezo
wa mwalimu Arsene Wenger
Wengi mtakubaliana na mimi jinsi Arsene Wenger
alivyo wabadilisha wachezaji wake wengi kutoka kua wachezaji wa kawaida hadi
kuwa wachezaji wa kiwango cha dunia kama Aaron Ramsey na wenzake huku akiwa na
uwezo mkubwa wa kuwa saikoloji wachezaji wake.
0 comments:
Post a Comment