Saturday, September 13, 2014

Wagonga Nyundo wa Mbeya, Mbeya City fc 

Na Baraka Mpenja
HATIMAYE kila kitu kimekwenda sawa!. Hivyo ndivyo unaweza kusema baada ya Vipers FC (Zamani Bunamwaya) kuwasili jijini Mbeya asubuhi hii kuikabili Mbeya Cit fc katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki unaopigwa jioni ya leo uwanja wa Sokoine.

Afisa habari wa Mbeya City fc, Dismas Ten ameimbia MPENJA BLOG kuwa, Vipers fc inayoshiriki ligi kuu nchini Uganda imetua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe kutokea Dar es salaam majira ya saa 1:45 asubuhi kwa ndege ya shirika la Fastjet.

Dismas amesema baada ya kuwasili, wachezaji na viongozi wa timu hiyo wamepumzika na wana matarajio ya kuwahi zaidi uwanjani kupasha moto misuli kabla ya mechi kuanza saa 10:00 jioni.

“Vipers FC wameelezea furaha yao kufika Mbeya kwa mara ya kwanza na wameahidi kuonesha mchezo mzuri dhidi ya Mbeya City. Kikubwa ni kwamba tusubiri tu jioni ili tuone kile walichoandaa”.

“Nilikuwa nazungumza na katibu wao anaitwa Dominick ambaye amesema wamejiandaa vizuri”.

Afisa habari huyo aliongeza kuwa hamasa kuelekea mechi hiyo ni kubwa kwasababu wapenzi wa soka mkoani humo wanapenda timu yao na wamekuwa wakihamasika pale inapocheza.

“Tuna imani kuwa mashabiki wengi watajitokeza kuiona hii mechi na hasa ukizingatia kuwa kiingilio ni cha chini kabisa ambacho ni shilingi 30,000”.

Aidha, Dismas alisema kocha Juma Mwambusi hana wasiwasi na mechi hiyo na ameeleza kuwa kikosi kipo fiti tayari kwa mechi hii.

“Mwalimu amesema atajaribu kutumia mifumo yote atayotumia katika michuano ya ligi kuu msimu ujao”. Alifafanua Dismas.

Baada ya mechi ya leo, kikosi cha Mbeya City fc kitarudi tena kambini kujiandaa na mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya JKT Ruvu, septemba 20 mwaka huu uwanja wa Sokoine Mbeya.



0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video