Lionel Messi na Luis Suarez walikuwa na tabasamu kubwa wakijiandaa dhidi ya Malaga na Indonesia
LUIS Suarez ataichezea Barcelona B kesho mchana katika mechi ya kikosi cha vijana chini ya miaka 19 dhidi ya Indonesia.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay hataweza kuichezea Barcelona katika mchezo wa La Liga dhidi ya Malaga kesho jumatano, lakini anaruhusiwa kuichezea katika mechi za kirafiki.
Nyota huyo wa zamani wa Liverpool ataikosa tena nafasi ya kuichezea timu yake mechi ya mashindano kwasababu anatumikia kifungo hadi oktoba 24.
Neymar anatarajia kuongeza magoli zaidi baada ya kufunga dhidi ya Levante mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kocha mkuu wa Barcelona, Luis Enrique, wa pili kutoka kushoto akijadili mbinu za mpira na wasaidizi wake
Enrique alisema: 'Luis Suarez atacheza mechi ya kirafiki ya timu B. Anahitaji kucheza, anataka kupata kasi ya mechi".
0 comments:
Post a Comment