
Louis van Gaal na Ryan Giggs walioneka kushitushwa na kipigo dhidi ya Leicester
IMETAARIFIWA kuwa Louis van Gaal aliwacharukia wachezaji wa Manchester United kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kufuatia kipigo cha 5-3 kutoka kwa Leicester.
Van Gaal aligeuka mbogo akiwalaumu wachezaji wake kwa kupoteza uongozi wa 3-1 na kumaliza mechi kwa kipigo kizito.
Kocha huyo mwenye heshima ya kutokuwa na hasira na wachezaji wake, aliwakalipia waziwazi baada ya kufungwa kwa mara ya pili katika michuano ya ligi kuu England.

Wachezaji wa Manchester United United wakionekena wamekata tamaa baada ya kufungwa goli la tano katika uwanja wa King Power

Wachezaji wa United wakishangilia bao la Ander Herrera lililowafanya wawe mbele kwa mabao 3-1
United walipata kipigo cha aibu na kumuacha Van Gaal na hasira za ajabu.
Van Gaal alikuwa na Radamel Falcao, Wayne Rooney na Van Persie katika kikosi kilichoanza, lakini baadaye alilalamika akisema: "Tuna wachezaji wengi ambao hawatafuti magoli."
0 comments:
Post a Comment