Nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney alitolewa nje kwa kadi nyekundu
LOUIS van Gaal amejiondoa katika mjadala ulioanza kuhusu Wayne Rooney ambapo watu wanahoji kama anafaa kuwa nahodha wa Manchester United kufuatia kuoneshwa kadi nyekundu iliyotokana na kumfanyia faulo ya kinyama mchezaji wa West Ham jana Old Trafford.
Rooney alioneshwa kadi nyekundu ya sita katika maisha yake ya soka baada ya kumpiga teke Stewart Downing na kuwaacha wenzake wakiwa 10 kulinda ushindi wa 2-1 kwa zaidi ya nusu saa.
Lakini Van Gaal amepotezea maneno yanayoendelea kuwa yawezekana alifanya makosa kumteua Rooney kuwa nahodha, lakini Mholanzi huyo ametoa hoja kuwa kitendo hicho ni cha kawaida katika mpira wa miguu.
Rooney akioneshwa kadi nyekundu na mwamuzi Lee Mason katika dakika ya 59 baada ya kumfanyia faulo mbaya Downing (kushoto aliyelala)
0 comments:
Post a Comment