Neymar akipongezwa na Lionel Messi baada ya kupiga hat-trick katika dimba la Nou Camp
HATARI sana! Lionel Messi amevuka mabao 400 katika maisha yake ya soka ngazi ya klabu na Neymar amepiga 'hat-trick' ya kwanza Barcelona ikishinda 6-0 dhidi ya Granada na kukaa kileleni mwa La Liga.
Muargentina huyo sasa amefikisha mabo 401 katika klabu yake na mabao 524 timu ya Taifa, akiwa na umri wa miaka 27.
Mabao matatu ya Neymar na mawili ya Messi yamemfariji sana kocha Luis Enrique kuelekea mechi ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya PSG jumanne ya wiki kesho.
Mshambuliaji wa Brazil, Neymar akiachia shuti kali kuifungia Barcelona bao la kuongoza dhidi ya Granada
Lionel Messi akifanya mambo yake
Messi akishangilia mbele ya mashabiki waliofurika Nou Camp kukamilisha ushindi wa 6-0
0 comments:
Post a Comment