Mbrazil, Andrey Coutinho (katikati) aliinyoa Prisons goli moja katika ushindi wa Yanga wa 2-1 uwanja wa Taifa
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
LIGI kuu soka Tanzania bara msimu huu inaonekana
kuwa na changamoto tangu mapema.
Mpaka sasa zimechezwa raundi mbili, lakini timu
zimenyoana si mchezo. Hebu nikukumbushe namna zilivyonyoa, zilivyonyolewa na
kunyoana.
Stand United ikitokea kunyolewa 4-1 na Ndanda fc
uwanja wa Kambarage Shinyanga nayo ilimnyoa Mgambo JKT 1-0 uwanja wa CCM
Mkwakwani, Tanga.
Prisons ikitokea kuinyoa Ruvu Shooting 2-0 uwanja
wa Mabatini, Pwani nayo jana ilinyolewa 2-1 na Yanga.
Yanga akitokea kunyolewa 2-0 na Mtibwa Sugar
uwanja wa Jamhuri Morogoro, ilifanikiwa kuinyoa Prisons jana uwanja wa Taifa.
Kagera Sugar ikitoka kunyolewa 1-0 na Mgambo JKT mechi
ya ufunguzi Mkwakwani Tanga, nayo iliinyoa JKT Ruvu 2-0 jana, Azam Complex,
Chamazi.
Coastal Union ikitokea kunyoana 2-2 na Simba,
ilinyolewa 1-0 na Mbeya City iliyoshindwa kunyoana na JKT Ruvu mechi ya
ufunguzi.
Polisi Morogoro ikitokea kunyolewa 3-1 na Azam fc
uwanja wa Azam Complex Chamazi, ilinyoana 1-1 na Simba jumamosi iliyopita
uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Ndanda fc iliyotoka kuinyoa Stand United 4-1
uwanja wa Kambarage Shinyanga, nayo ilinyolewa 3-1 na Mtibwa Sugar uwanja wa
Manungu, Complex.
Ruvu Shooting yenyewe imenyolewa mara mbili( 2-0 kutoka
Prisons, 2-0 dhidi ya Azam fc).
Timu pekee ambazo zina wembe mkali ni Mtibwa Sugar
na Azam fc.
Mtibwa Sugar wamezinyoa timu mbili. Waliinyoa
Yanga 2-0 na wikiendi iliyopita wakainyoa Ndanda fc 3-1.
Azam fc nao wamezinyoa timu mbili. Waliinyoa
Polisi Morogoro 3-1 na juzi wameinyoa 2-0 Ruvu Shootings.
Ngoja tusubiri kama timu zitaendelea kunyoa,
kunyolewa na kunyoana kwa staili hii….
0 comments:
Post a Comment