Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
RAUNDI ya pili ya ligi kuu soka Tanzania bara
inatarajia kuendelea wikiendi hii kwa timu zote 14 kushuka dimbani.
Kesho jumamosi (septemba 27 mwaka huu), Wekundu wa
Msimbazi, Simba sc wenye kumbukumbu ya kutoka sare ya 2-2 na Coastal Unioni
wikiendi iliyopita watakuwa nyumbani uwanja wa Taifa, Dar es salaam kuchuana na
Polisi Morogoro.
Katika mechi ya ufunguzi, septemba 20, Polisi Moro
walifungwa mabao 3-1 na Mabingwa watetezi, Azam fc.
Mtibwa Sugar wenye kumbukumbu ya kuifunga Yanga
2-0 katika mechi ya ufunguzi uwanja wa Jamhuri wikiendi iliyopita
wataikaribisha Ndanda fc ya Mtwara iliyoshinda 4-1 dhidi ya Stand United katika
mechi ya ufunguzi uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Azam fc walioshinda 3-1 mechi iliyopita
wataikaribisha Ruvu Shootings iliyofungwa 2-0 katika mechi ya ufunguzi uwanja
wa Mabatini, Pwani.
Mbeya City fc iliyotoka 0-0 na JKT Ruvu itakuwa
uwanja wa nyumbani wa Sokoine kwa mara nyingine kuwakaribisha Wagosi wa Kaya,
Coastal Union ya Tanga.
Coastal wao walitoka sare ya 2-2 na Simba katika
mechi ya ufunguzi iliyopigwa wikiendi iliyopita uwanja wa Taifa.
Mgambo JKT walioshinda 1-0 mechi iliyopita dhidi
ya Kagera Sugar watakuwa nyumbani CCM Mkwakwani Tanga kuchuana na Stand United
waliotandikwa 4-1 na Ndanda fc katika mechi ya ufunguzi, uwanja wa Kambarage.
Ligi hiyo itaendelea jumapili (septemba 28) ambapo
mechi mbili zitapigwa.
Yanga wenye kumbukumbu ya kupigwa 2-0 mechi
iliyopita uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar watakuwa
nyumbani uwanja wa Taifa, Dar es salaam kuwakaribisha Prisons walioshinda 2-0
mechi iliyopita dhidi ya Ruvu Shooting.
JKT Ruvu waliotoka 0-0 na Mbeya City fc Sokoine
Mbeya, watakuwa nyumbani Azam Complex kuchuana na Kagera Sugar waliotandikwa
1-0 katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Mgambo JKT.
0 comments:
Post a Comment