Diego Costa ametisha sana tangu alipojiunga na Chelsea
JOSE Mourinho anaamini Diego Costa sio mchezaji wa kawaida baada ya kupiga mabao matatu katika mechi ya jana ya ligi kuu dhidi ya Swansea.
Mabao hayo sasa yamemfanya Costa afikishe magoli saba katika mechi nne tangu aliposajiliwa kwa paundi milioni 32 kutoka Atletico Madrid majira ya kiangazi mwaka huu.
Kocha wa Jose Mourinho amefurahishwa sana na kiwango cha Costa.
"Kama timu inacheza vizuri lazima afunge magoli. Saba katika mechi nne, labda amezidisha," alisema kocha huyo baada ya kushinda mabao 4-2."Ni kitu kisichokuwa cha kawaida. Hatuwezi kutarajia kuwa baada ya mechi nane atakuwa na magoli 14."
"Ametulia kwenye timu. Timu ilijengwa kwa staili ya kusubiri mshambuliaji kama yeye na nadhani kila mtu anajua kuwa Chelsea haikufanya makosa kwa kutokwenda sokoni katika dirisha dogo la usajili, januari 2013"
0 comments:
Post a Comment