Saturday, September 27, 2014

Na Baraka Mpenja, Dar es salam

0712461976

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania bara jioni ya leo wanawakaribisha maafande wa Ruvu Shooting katika mechi ya raundi ya pili ya ligi kuu itakayopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es salaam.

Wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Polisi Moro wikiendi iliyopita, Azam wanakutana na Ruvu Shooting iliyochapwa 2-0 na Prisons mechi ya ufunguzi (septemba 20 mwaka huu) uwanja wa Mabatini, Pwani.

Shooting imekuwa ikitoa upinzani mkubwa katika michuano ya ligi kuu, lakini rekodi ya msimu uliopita inaonesha wazi kuwa walikuwa dhaifu mbele ya Azam fc, nyumbani na Ugenini (walifungwa mabao 6 bila majibu kwa mechi zote mbili).

Azam fc kwa asilimia zote walitangaza ubingwa wao katika mechi dhidi ya Shooting uwanja wa Mabatini wakishinda 3-0.

Leo hii Maafande hawa chini ya kocha Mkenya, Tom Alex Olaba wanaingia  wakiwa na hasira za kutaka kulipa kisasi, lakini changamoto itakuwa kubwa sana.

Azam fc wameendelea kuwa bora wanapocheza uwanja wa nyumbani, hata msimu uliopita walikuwa wanatoa dozi kali Azam Complex.

Mazingira ya uwanja huo ni rafiki kwa wachezaji wa Azam fc. Muda wote wanafanya mazoezi hapo na inapofika siku ya mechi wanamalizia kazi tu.

Kushinda Chamazi ni ngumu ,  hivyo Ruvu Shooting wanatakiwa kujipanga barabara.

Kikosi cha kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog kilianza kwa kupoteza kikombe cha Ngao ya Jamii, septemba 14 mwaka huu kufuatia kufungwa 3-0 na Yanga.
Didier Kavumbagu (kushoto) atafunga leo tena ?

Katika mechi hiyo, Azam hawakucheza vizuri, walizidiwa ujanja na Yanga, walipoteza mechi kihalali, lakini mechi ya ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Polisi Moro walionekana kuimarika upya na kuwa katika morali ya hali ya juu.
Kinachowabeba wachezaji wa Azam ni mazingira bora ya klabu hiyo. Kwa asilimia kubwa wamekamilika kiuchezaji. Wana utimamu wa mwili, wako sawa kiufundi, kimbinu na kisaikolojia.
Lakini wameendelea kufanya makosa ya uwanjani kama sehemu ya mchezo. Mpira wa miguu ni mchezo wa makosa.

Makosa yapo, yataendelea kuwepo na ndio kazi ya makocha kupunguza na kufuta makosa hayo duniani kote.
Katika mechi ya leo Azam wataendelea kuwakosa washambuliaji wake wawili, Nahodha, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ na Mhaiti Leonel Saint Preux. Hata hivyo, Kipre Tchetche na Didier Kavumbagu wana uwezo wa kufunga magoli.

Omog anaweza kumuanzisha mchezaji yeyote ambaye yuko fiti. Azam wana kikosi kikubwa na kila mchezaji anaweza kuonesha kile alichoagizwa.

Mechi iliyopita, Aishi Manula alianza badala ya Mwadini Ali. Alicheza vizuri na leo hii Omog anaweza kumpanga tena kama hana tatizo lolote.

Shomari Salum Kapombe anaweza kucheza beki ya kulia, kinda Gadiel Michael kushoto au Erasto Nyoni.

David Mwantika na Aggrey Morris wana asilimia zote kuanza nafasi ya mabeki wa kati. Morris amekuwa katika ubora wake na faida yake ni kuweza kupanda kuongeza mashambuliaji.

Beki huyo alipanda mara kadhaa kwenye mechi dhidi ya Polisi na kufanikiwa kufunga goli moja kati ya nafasi kadhaa alizopata.

Morris ni beki wa kisasa. Anaweza kuisaidia timu kufunga na anaweza kufanya hivyo kutokana na safu bora ya kiungo ya Azam.

Bolou Michael ni kiungo bora wa ulinzi, Salum Abubakary ‘Sure Boy’ ni kiungo mzuri wa uchezeshaji. Lakini pembeni Himid Mao na Tchetche wamekuwa na uwezo mzuri wa kuziba mianya ya mashambulizi kutoka kwa upinzani pale Morris anapopanda juu.

Kama hatachungwa leo, beki huyu wa kati, raia wa Zanzibar anaweza kufunga tena.

Kutokana na ukubwa wa kikosi cha Azam fc, kumewafanya wawe na uwezo mkubwa wa kupata matokeo, lakini ligi imebadilika siku hizi.

Ruvu Shooting ni timu pinzani na msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya Sita kati ya timu 14. Kikosi chao kimesukwa upya, kimesheheni vijana wadogo na wakongwe.

Kilizidiwa na Prisons mechi iliyopita na kuifungwa 2-0, lakini ukirejea katika mechi za majaribio ikiwemo waliyofungwa 1-0 na Azam fc uwanja wa Azam Complex, walicheza vizuri sana.

Leo wanakabiliana na timu bora ikiwa nyumbani kwake. Ni ngumu sana kupata matokeo, hata historia haiwatendei haki.

Mpira wakati fulani hauheshimu historia, lakini kuchomoka Chamazi sio jambo jepesi hata kidogo.


Kwa upande wangu, nawapa Azam fc asilimia 80 ya kuibuka na ushindi, japokuwa mpira una matokeo ya tofauti.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video