Jack Wilshere amemtuliza, Mfaransa Arsene Wenger
ARSENE Wenger amesisitiza kuwa Jack Wilshere amezima ukosoaji wake baada ya kufunga bao dhidi ya Manchester City.
Mchezaji wa zamani wa England na Manchester United, Paul Scholes amekuwa akihoji mara kwa mara, kwanini maendeleo ya Wilshere sio mazuri tangu alipocheza mechi ya kwanza mwaka 2008?
Kijana huyo mwenye miaka 22 alijibu mapigo kwa kuonesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya mabingwa watetezi, akimlipa Sergio Aguero aliyeifungia Man City bao la kuongoza.
Wilshere alimtungua kwa ustadi mkubwa kima Joe Hart, kabla ya Alexis Sanchez kumpeleka maboya na kuandika bao la pili.
Kichwa cha dakika za mwisho cha Martin Demichelis kiliiokoa Man City na kutoka sare ya 2-2 uwanja wa Emiratse, lakini Wilshere ndiye alikuwa kivutio katika mechi hiyo.
"Sehemu nzuri ya kujibu ukosoaji ni ndani ya uwanja," alisema Wenger ambaye alimtetea kwa mara nyinge Mesut Ozil aliyeonekana kuchemsha kwenye mechi hiyo.
"Hiki ndicho alifanya Jack, lakini siamini kama tunaweza kuelezea kiwango chake kwa kuangalia ukosoaji wa Paul Scholes.
"Lakini unatakiwa kujibu unapokuwa mbele ya mashabiki. Unakubali kukosolewa, nenda uwanjani na onesha kuwa una kipaji"
"Kitu cha msingi ni kuonesha ni jinsi gani unaweza. Jack alimalizia vizuri na kumfunga kipa anayemjua vizuri. Nimefurahi sana kwa jinsi alivyomalizia kazi"
Wilshere alibadilishana pasi na Mesut Ozil kabla ya kumfunga Joe Hart
0 comments:
Post a Comment