Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Taifa
Stars, Seklojo Johnson Chambua ameseme mechi ya Ngao ya Jamii kuashiria
kuzinduliwa kwa pazia la ligi kuu soka Tanzania bara itakayopigwa jioni ya leo (septemba
14 mwaka huu) uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baina ya Azam fc na Yanga
itatoa picha halisi ya ligi kuu itakavyokuwa msimu ujao unaotarajia kuanza
septemba 20.
Akizungumza na MPENJA BLOG mchana huu, Chambua
amesema timu zote zina wachezaji wazuri na uwezo wa kifedha, hivyo nguvu inaelekeana
kwa asilimia kubwa.
Chambua alifafanua kuwa hategemei kuona wachezaji
wakicheza kibinafsi bali kitimu zaidi, wakipanga mashambulizi kwa pamoja na
kujihami kwa ustadi mkubwa.
“Kwangu mimi nafikiri itakuwa mechi moja nzuri na
yenye kusisimua kwasababu ukiangalia timu zote mbili zimejiandaa vizuri zaidi,
zina wachezaji wazuri, zina uwezo wa kifedha, kwahiyo namna ninavyoiangalia
hii, itakuwa ya upinzani sana na itatoa picha ni timu ipi imejiandaa vizuri kwa
ajili ya msimu huu.” Alisema Chambua.
“Hizi ni timu kubwa, zitegemei kuona wachezaji
wakicheza kibinafsi, nategemea kuona timu inashambulia vipi, inajihami vipi
katika masuala ya kimfumo. Natarajia kuona timu zimejipanga vipi na kuwaonesha
Watanzania kuwa ziko imara kiasi gani.”
Kuhusu Azam fc, Chambua alikiri kuwa ni timu
inayobadilika kila siku na sasa imeimarika zaidi.
“Azam sasa hivi imeimarika, ilivyocheza Kagame
kila mtu aliona kuwa timu imebadilika, natarajia mechi ngumu, lakini matokeo
yatapatikana ndani ya uwanja na si nje ya
uwanja. Kiujumla itakuwa mechi nzuri sana”.
“Kwa walimu wote wawili itakuwa kipimo kizuri na
kwa matokeo yoyote yale, walimu watapata picha kabla ya ligi kuanza na
wachezaji watavyocheza watatoa sura halisi ya ligi itakavyokuwa”.
Azam fc wataanza kampeni ya kutetea ubingwa dhidi
ya Polisi Morogoro uwanja wa Chamazi, septemba 20, wakati siku hiyo Yanga
watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment