Diego Costa ameonesha ubora wake wa kufumania nyavu baada ya kufunga mabao matatu dhidi ya Swansea City.
KAMA Diego Costa alikuwa na bei ya Paundi milioni 320, bado alistahili thamani hiyo.
Ni kitu gani hiki Mhispania huyu ameleta katika ligi England?
Amefunga magoli saba katika mechi nne tangu awasili Chelsea akitokea Atletico Madrid kwa dau la paundi milioni 32.
Amefikisha idadi hiyo baada ya kufunga mabao matatu 'Hat-tric' dhidi ya Swansea City jioni ya leo, Chelsea ikishinda 4-2 Stamford Bridge.
Kwa asilimia 100 ni rekodi nzuri mno kwa nyota huyu aliyetamba na Atletico msimu uliopita.
Ushindi huu umewasha taa nyekundu kwa wapinzani wa ubingwa wa EPL na umeonesha kuwa timu ya Jose Mourinho ni hatari msimu huu.
Mshambuliaji wa zamani wa Queens Park Rangers,Loic Remy akifunga bao katika mechi ya kwanza na kuufanya ubao wa matangazo kusomeka 4-1
MATOKEO YA MECHI ZILIZOMALIZIKA HAYA HAPA
ENGLAND: Premier League | |||||||
04:45 | Finished | Arsenal | 2 - 2 | Manchester City | |||
07:00 | Finished | Chelsea | 4 - 2 | Swansea | |||
07:00 | Finished | Crystal Palace | 0 - 0 | Burnley | |||
07:00 | Finished | Southampton | 4 - 0 | Newcastle Utd | |||
07:00 | Finished | Stoke City | 0 - 1 | Leicester | |||
07:00 | Finished | Sunderland | 2 - 2 | Tottenham | |||
07:00 | Finished | West Brom | 0 - 2 | Everton | |||
09:30 | 13 | Liverpool | 0 - 1 | Aston Villa |
0 comments:
Post a Comment