Chelsea wamewasiliana na 'Rugby Football Union' wakiomba kutumia uwanja wa Twickenham kwa miaka kadhaa.
CHELSEA imeanza mchakato wa kuomba kuhamia kwa muda katika uwanja wa Twickenham kutokana na mipango ya kutaka kuboresha uwanja wa Stamford Bridge.
Tayari Chelsea wameshaanza mawasiliano na mamlaka inayohusika na usimamizi wa uwanja huo ya 'Rugby Football Union.
RFU wamethibitisha kuwa klabu hiyo kubwa ya ligi kuu England imeomba kutumia uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 82,000.
Mwezi juni mwaka huu, Chelsea walitangaza kupanua uwanja wao, lakini hawakutaja muda wa kuanza kazi hiyo.
Kulikuwa na taarifa kuwa klabu hiyo inaweza kutafuta eneo lingine la kudumu la nyumbani, lakini London inapewa kipaumbele.
Chelsea wanaweza kucheza mechi za nyumbani kwa muda mfupi katika uwanja wa Twickenham
Siku za nyuma klabu zilikataliwa kutumia uwanja wa Twickenham uliopo Scotland .
Mkurugenzi wa RFU, Francis Baron alikataa mwaka 2001, wakati Fulham ikitafuta uwanja wa muda wa nyumbani.
Baron alisema: "Hatujavutiwa na suala hilo".
Taarifa ya RFU ilisema : "Tumekuwa na mawasiliano na mashirika mengi , nje na ndani ya michezo kuhusu namna ya kutumia uwanja huo ambao tunaamini ni wa kiwango cha dunia. Tumepata maombi kutoka Chelsea FC, lakini hatujafanya mazungumzo yoyote kuhusu hilo"
0 comments:
Post a Comment