Boniface Pawasa |
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BEKI kisiki wa zamani wa Simba na Timu ya Taifa ya
Tanzania, ‘Taifa Stars’, Boniface Pawasa amesema mechi ya Ngao ya Jamii
inayopigwa leo jioni uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baina ya Azam fc na
Yanga haitabiriki hata kidogo.
Pawasa amezungumza na MPENJA BLOG muda mfupi
uliopita na kueleza kuwa kitakwimu, Azam wapo katika nafasi nzuri zaidi ya
Yanga kwasababu timu yao imekaa pamoja kwa muda mrefu, kuliko Yanga chini ya
Marcio Maximo.
“Ni mechi ambayo huwezi kuitabiri haraka, lakini
ukiangalia takwimu na uzoefu, unaweza kuona Azam wapo katika nafasi nzuri,
kwasababu timu yao imeweza kuelewana, juzi juzi ilikuwa katika mashindano ya
Kagame. Kwahiyo tayari Azam imeshapata mfumo kwa vile mwalimu wao amekuwa na
timu kwa muda mrefu.” Alisema Pawasa.
“Wasiwasi ni mabadiliko ya mfumo wa Yanga, lakini
najua Maximo ni mwalimu anayeujua vizuri mpira wa Tanzania, Maximo ni mwalimu mshindani,
kwahiyo naamini ana kikosi kizuri, lakini wasiwasi wangu ni timu kombinesheni.”
“Sijaona kama wana kombinesheni bora kuweza kuwapa
presha Azam fc, kwamaana nimewaangalia Azam Kagame Cup, ni timu ambayo imeanza
kusifika na imeonesha njia. Kwa Yanga mwalimu ana muda mfupi na timu, lakini siwezi kusema ndio
sababu ya kufanya vibaya”
“Wachezaji ni walewale na kuna wengine wameongezeka,
sema mwalimu amekuja na mfumo mpya, kuna mabadiliko, kuna wachezaji walikuwa
hawapati nafasi, sahizi wanapata nafasi, leo hii wanacheza mechi ya presha”
“Kwa upande wangu, naangalia uzoefu, takwimu,
naona Azam wako vizuri kuliko Yanga”.
0 comments:
Post a Comment