Hector Bellerin (kulia) alikuwa miongoni mwa wachezaji vijana wa Arsenal dhidi ya Southampton
ARSENE Wenger ametetea maamuzi yake ya kuwatumia vijana wadogo katika safu ya ulinzi Arsenal ikifa 2-1 mbele ya Southampton na kutupwa nje ya kombe la Capital One.
Goli la penalti la Dusan Tadic, likifuatiwa na la Nathaniel Clyne umbali wa mita 30 liliwapa ushindi Southampton katika uwanja wa Emirates baada ya Alexis Sanchez kuifungia Arsenal bao la kuongoza kwa mpira wa adhabu ndogo.
Beki wa Arsenal iliyeimarika kutoka kwenye majeruhi Mathieu Debuchy na Nacho Monreal hawakuwepo jana na Wenger alisema baada ya kufungwa kuwa Per Mertesacker na Kieran Gibbs walikuwa tayari kuanzia benchi tu.
Wachezaji wa Arsenal waliocheza jana ni Hector Bellerin, Calum Chambers, Isaac Hayden na Francis Coquelin -ambao ni viungo wa kati kiasilia.
Wenger alisema: "Tulikosa uzoefu sehemu ya nyuma. Tulijitahidi sana na tumeumia kushindwa kufunga magoli kipindi cha pili."
"Tuna matatizo madogo safu ya ulinzi, ndiyo, kwasababu ya majeruhi. Unakaa na kutafakari: Gibbs ana matatizo ya nyama za paja na huwezi kumtumia, Mertesacker naye ana matatizo, hatukuwa na jinsi.
"Nadhani kama tumepoteza mechi usiku huu (jana) sio kwasababu ya Hayden, Chambers wala Coquelin. Lazima uwe mkweli.
0 comments:
Post a Comment