Arsene Wenger amevutiwa na ushirikiano baina ya Mesut Ozil na Danny Welbeck
ARSENE Wenger amesema safu yake ya ushambuliaji imekuwa na nguvu baada ya Mesut Ozil na Danny Welbeck kuwa na ushirikiano mzuri na anaamini watafanya vizuri katika mechi ya kesho ya watani wa jadi wa London, dhidi ya Tottenham.
Welbeck aliifungia Arsenal goli lake la kwanza katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Aston Villa wikiendi iliyopita na siku hiyo Ozil alionesha kiwango cha juu katika majukumu ya namba 10 akishirikiana vizuri na mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United.
"Alicheza (Ozil) vizuri sana na walielewana sana na Danny Welbeck," alisema Wenger. " Ni patinashipu nzuri kwasababu wanapeana mipira vizuri na kufunga. Ni jambo la kuvutia".
Welbeck alifunga goli lake la kwanza akiichezea Arsenal akisajiliwa kutoka Manchester United majira ya kiangazi mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment