Saturday, September 13, 2014


ARSENAL wanaikaribisha Manchester City katika mechi ya ligi kuu England itakayopigwa Emirates mapema majira ya saa 8:45 mchana.
Msimu uliopita, Arsenal walitandikwa mabao 6-3 na kikosi cha Manuel Pellegrini katika uwanja wa Etihad, na leo hii wanaingia uwanjani wakitaka kulipa kisasi.
Itakuwa ni vita kali Emirates, nani ataibuka mbabe? dakika tisini zitaamua.
Mechi nyingine itawakutanisha Chelsea dhidi Swansea katika dimba la Darajani.
Crystal Palace watakuwa nyumbani kuchuana na Burnley, wakati Southampton nao watakuwa nyumbani dhidi ya Newcastle.
Stoke City watakuwa wenyeji wa Leicester na Sunderland watakuwa dimba la nyumbani kuchuana na Tottenham.
Nao West Brom watakuwa uwanja wa nyumbani kukabliana na Everton.
Majogoo wa jiji, Liverpool watakuwa nyumbani Anfield kuoneshana kazi na Aston Villa.
Ligi hiyo itandelea kesho ambapo Manchester United watakuwa na kibarua kizito Old Trafford kuchuana na QPR.
Mtandano huu utakuletea matokeo ya mechi zote...kaa hapa hapa...

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video