Rabiot amecheza kila mechi ya timu ya Taifa ya Ufaransa
ARSENAL hawana masihara sasa!. Wanahitaji mazungumzo na PSG kuhusu kumsajili kiungo Adrien Rabiot ambaye anamaliza mkataba wake majira ya kiangazi mwaka huu na anaweza kuongea na klabu za nje kuanzia mwezi januari.
Vyombo vya habari vya Ufaransa vilimhusisha Rabiot kujiunga na washika bunduki mapema majira ya kiangazi mwaka huu, lakini sasa inaaminika kuwa Arsene Wenger amevutiwa naye baada ya kuonesha kiwango kizuri akiwa na timu ya U21 ya Ufaransa.
Nyota huyo mwenye miaka 19 kwasasa ana mkataba na PSG mpaka mwaka 2015, lakini ameshindwa kuongeza mwingine na kocha Laurent Blanc.
0 comments:
Post a Comment