NYOTA mpya wa Manchester Unite, Angel di Maria alishangilia goli lake katika ligi ya England dhidi ya QPR kwa kuonesha ishara ya moyo akitumia mikono yake.
Mchezaji mwenzake wa zamani wa Di Maria akiwa Real Madrid, Gareth Bale, ambaye alivunja rekodi ya usajili Santiago Bernabeu, pia alitumia ishara kama hiyo ya moyo baada ya kuifungia klabu na nchi yake.
Bale alifanya ishara hiyo juni 2013 ambapo alimaanisha mapenzi kwa kipenzi chake Emma Rhys-Junes.
Gareth Bale (picha ya juu zaidi) na Angel di Maria (pichani juu) alitumia ishara ya moyo baada ya kufunga goli lake
Angel di Maria akishangalia na ishara yake baada ya kuifungia United bao dhidi ya QPR katika dimba la Old Trafford
Nyota huyo wa Manchester United akishangilia mbele ya mashabiki wake wapya
Angel di Maria na Gareth Bale msimu uliopita walikuwa wanaichezea klabu ya Real Madrid
Gareth Bale alitumia shepu ya moyo wakati akitambulishwa Santiago Bernabeu
Nyota wa zamani wa Tottenham alipigwa picha akitumia ishara hiyo akiwa na timu ya Taifa ya Wales
Hata hivyo, Di Maria alitumia ishara ya moyo kushangilia akimaanisha mapenzi ya Mpira, kama ale, kiungo huyo wa Manchester United amekuwa akifanya hivyo tangu alipokuwa Benfica.
Di Maria alitumia ishara kama hiyo Desemba 2009 katika ushindi wa Benfica wa 2-1 dhidi ya AEK Athens, wakati Bale kwa mara ya kwanza alifanya hivyo mwaka 2010.
Mashabiki wa Manchester United wana matumaini ya kuona ishara nyingi za ushangiliaji za Di Maria wakati huu akiwa Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment