
Fundi: Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Mario Mandzukic akifunga bao la kuongoza dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa marudiano wa 'Spanish Super Cup'
REAL Madrid wameanza vibaya msimu mpya baada ya jana kupigwa bao 1-0 na mahasimu wao Atletico Madrid katika uwanja wa Vicente Calderon na kupoteza kombe la 'Spanish Super Cup'.
Mechi ya kwanza Santiago Bernabeu timu hizo zilitoka sare ya 1-1, hivyo Atletico kushinda kwa wastani wa mabao 2-1.
Bao pekee la ushindi wa Atletico lilitiwa kambani na mshambuliaji mpya ambaye unaweza kusema amerithi mikoba ya Diego Costa, Mario Mandzukic.
Msimu uliopita, kikosi cha Diego Simeone kiliwazidi kete Real Madrid na kutwaa kombe la ligi kuu maarufu kama La Liga, sasa wamewashinda katika kombe la 'Spanish Super Cup'
Real Madrid wametumia fedha nyingi kununua wachezaji nyota katika kombe la dunia lililopita, lakini jambo la kuwaunganisha na kuwafanya wacheze kitimu ni muhimu zaidi.
Carlo Ancelotti ana kazi kubwa zaidi kwasababu jana walijikuta wakiwa nyuma kwa bao 1-0 katika sekunde ya 80 (sawa na dakika 2) na walishindwa kutafuta upenyo wa kusawazisha.
Kikosi cha Atletico Madrid: Moya; Juanfran, Godín, Miranda, Siqueira; Tiago, Gabi; Koke, Raul García, Griezmann (Jiminez 73); Mandzukic
Wachezaji wa akiba: Oblak, Suarez, Rodriguez, Ansaldi, Niguez, Gimenez
Kikosi cha Real Madrid: Casillas; Carvajal, Varane, Ramos, Coentrao (Marcelo 70); Modric, Kroos (Ronaldo 45), Xabi Alonso; James (Isco 65), Benzema, Bale
Wachezaji wa akiba: Navas, Pepe, Arbeloa, Illarra
Shujaa wa goli: Mshambuliaji wa Atletico, Mario Mandzukic akinyanyua kombe la Super Cup baada ya kuifunga Real Madrid jana

Mabingwa: Atletico wameanza msimu kwa kuwazidi kete mahasimu wao na kutwaaa kombe


Shangwe: Nyota wa Atletico, Mario Mandzukic (katikati) akishangalia bao lake la sekunde ya pili dhidi ya Real Madrid katika dimba la Vicente Calderon
0 comments:
Post a Comment