Mabingwa: Nyota vijana wa Ujerumani wakishangalia baada ya kutwaa taji kwa kuifunga Ureno bao 1-0 katika mchezo wa fainali.
Imechapishwa Agosti 1, 2014, saa 3:42 asubuhi
KIZAZI kijacho cha soka cha Ujerumani kimefuata nyayo za kaka zao kwa kushinda kombe lingine la Ulaya la vijana chini ya miaka 19.
Kiungo wa Hertha Berlin, alifunga bao pekee lililowapa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ureno huko Budepest.
Timu ya wakubwa ilitwaa kombe la dunia nchini Brazil kwa kuifunga Argentina bao 1-0 katika mechi ya fainali majira haya ya kiangazi nchini Brazil.
Sasa mataifa mengine yameanza kuwa na hofu baada ya kuona kizazi kijacho cha Ujerumani kinafanya mambo makubwa.
0 comments:
Post a Comment