Imechapishwa Agosti 1, 2014, saa 4:44 asubuhi
UEFA imethibitisha kuwa itachunguza tatizo la mashabiki
kuvamia uwanja katika mechi ya kufuzu ligi ya mabingwa barani Ulaya baina ya
Copenhagen na Dnipro Dnipropetrovsk.
Kipindi cha pili katika mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya tatu iliyopigwa uwanja Kiev Olympic
ilisimama kwa dakika 10 baada ya mashabiki wageni kutoka Uholanzi kuingia
uwanjani wakijihami kushambuliwa na kundi lingine, ambalo limeripotiwa kuwa
mashabiki wa Dnipro.
Timu hizo mbili zilikuwa zimeingia uwanjani kuanza kipindi
cha pili, lakini zilirudi tena kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati
maaskari wakijaribu kuwatoa mashabiki wa Ukraine waliovamia mashabiki wageni
ndani ya uwanja.
Baada ya wana Usalama kufanikiwa kuwatoa, mechi iliendelea
kama kawaida.
Mkurugenzi mkuu wa Copenhagen, Anders Horsholt aliwalaumu
Dnipro na uongozi wa uwanja kwa kushindwa kuimarisha ulinzi na taarifa kwa
vyombo vya habari kutoka UEFA inaeleza kuwa mamlaka inayohusika itafanya
uchunguzi wa tukio hilo.
“Uchunguzi imeanza dhidi ya mashabiki wa Dnipro
Dnipropetrovsk na kutojipanga kwa ulinzi,” Taarifa ilisomeka.
Mashabiki wa Dnipro wameripotiwa wakilaumu kuwa mashabiki wageni walinyanyua bendera ya
Urusi katika eneo lao kuwakebehi wanyeji, lakini taarifa ya Copenhagen kwenye
tovuti yake rasmi imekanusha tuhuma hizo.
0 comments:
Post a Comment