Anakwenda Merseyside? Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o anaweza kujiunga na Liverpool.
MCAMEROON, Samuel Eto'o yuko tayari kukamilisha usajili wa ghafla kujiunga na Liverpool.
Mario Balotelli aliwasili Merseyside jana kujaribu kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 16 kujiunga Anfield, lakini kama dili litashindikana, nafasi yake itachukuliwa na Mcameroon.
Inafahamika kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea alipimwa afya na Liverpool akiwa mjini Paris jana ijumaa.
Eto'o mwenye miaka 33 ambaye anaishi mji mkuu wa Ufaransa, amekubali dili la miezi 12 (mwaka mmoja) kujiunga na Liverpool na anasubiri kupanda ndege kwenda kusaini mkataba.
Eto’o aliripotiwa kuvutiwa na Everton kwa siku chache zilizopita, lakini kigezo cha kucheza ligi ya mabingwa kimemfanya aichague Liverpool.

Picha hii ya Mcameroon huyu alikuwa katika fainali za kombe la Dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.
0 comments:
Post a Comment