ImechapishwA Agosti 1, 2014, saa 5:12 asubuhi
SEYCHELLES
imeifuta mechi ya kesho jumamosi ya kufuzu fainali za mataifa ya Africa, AFCON
2015 nchini Morocco dhidi ya Sierra Leone kwasababu ya kuhofia virusi vya ugonjwa wa Ebola.
Hii
ina maanisha Seychelles imepoteza mechi na kuathiri nafasi yao katika
mashindano hayo.
Mapema
jana alhamisi ilithitishwa kwa BBC Sport kuwa Sierra Leone walizuiliwa kupanda
ndege kwenye uwanja wa ndege wa Nairobi Kenya ambapo wangesafiri moja kwa moja
kwenda Seychelles kucheza mechi ya marudiano.
Maamuzi
ya kuizua timu isisafiri yalichukuliwa na idara ya uhamiaji ya Seychelles,
ambao wanahusika kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola nchini mwao.
Maamuzi
hayo yalifuatiwa na taarifa kuwa rais wa Sierra Leone ametangaza kamati ya afya
ya dharura kupamaba na kuenea kwa ugonjwa huo.
Rais
wa chama cha soka cha Seychelles, Elvis Chetty aliiambia BBC: “Maamuzi ya
kupoteza mechi ni ya chama cha soka cha Seychelles”
“Napenda
kusema kwamba chama cha soka cha Seychelles kisilaumiwe kwa hili na chama cha Sierra
Leone.
“Tumechukua
maamuzi kwasababu ya ushauri uliotumwa na wizara ya afya ya Seychelles.
“Pia
tulipokea barua kutoka wizara ya uhamiaji ikisema kuwa haitaruhusu timu ya Sierra Leone kuingia nchini.
“Walituomba
kuahirisha mechi kwa muda usiojulikana, kwahiyo tumeona ni bora kupoteza kuliko
kuruhusu ichezwe.
Sierra
Leone iliyoshinda mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita, sasa
watapewa nafasi ya kucheza hatua inayofuata ya kufuzu.
Chetty
aliongeza: “Kwa mtazamo wa kimpira, kiukweli nimevunjwa moyo sana na hali hii.
Taifa lilikuwa linaisubiri sana mechi hii tofauti na miaka mingi ya nyuma.”
Seychelles
imeyaweka maamuzi yao katika maandishi
ili kuyapeleka shirikisho la soka barani Afrika, CAF na watapeleka
tangazo saa chache zijazo.
0 comments:
Post a Comment