Imechapishwa Agosti 1, 2014, saa 9:26 asubuhi
MALAGA imetangaza kumsajili kipa Guillermo Ochoa
ili arithi mikoba ya Willy Caballero.
Kipa huyo mwenye miaka 29, raia wa Mexico, alikuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na
klabu ya Ajaccio kumalizika mwishoni mwa msimu uliopita na alikuwa na ofa
nyingi kufuatia kuonesha kiwango cha ajabu katika fainali za kombe la dunia
majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil.
Ochoa ameamua kusaini Malaga ambao walikuwa
wanatafuta kipa namba moja baada ya Caballero kujiunga na Manchester City.
Malaga walitangaza jana jioni kuwa kipa huyo atatangazwa
rasmi kwenye mkutano na waandishi wa habari majira ya saa 11:00 jioni kwa saa
za Hispania.
Ochoa aliyeichezea nchi yake mechi 63, alianza
maisha yake ya soka huko America kabla ya kujiunga na Ajaccio mwaka 2011.
0 comments:
Post a Comment