Zinedine Zidane, kushoto, na Claude Makelele, kulia, wanaweza kuzilazimisha timu zao kucheza kama walivyocheza enzi zao.
Na Baraka Mpenja, Kwa msaada wa Mtandao
Imechapishwa Agosti 1, 2014, saa 12:00 jioni
Baada
ya mafanikio ya karibuni ya Pep Guardiola, Diego Simeone na Antonio Conte ,
inaonekana kizazi cha watu waliocheza mpira katika karne ya 20 na 21
kinazalisha makocha bora zaidi.
Zaidi
ya makocha watano wanaelekea kuzifundisha klabu kubwa na hapa chini ni
matarajio ya msimu wao wa 2014-15.
CLAUDE
MAKELELE, BASTIA
Wachezaji
wengi bado wanataka majina yao kuwa kama
mchezaji huyu wa zamani, lakini `Makelele’ alikuwa mchezaji mkubwa nchini
England kwasababu kiungo huyo wa Ufaransa alionesha kiwango kikubwa na klabu ya
Real Madrid na Chelsea.
Nyota
huyo alikuwa mahiri kuunganisha kiungo na kama ufundishaji wake unazingatia
namna alivyokuwa anacheza, Bastia nzuri na imara inatarajiwa.
Wanahitaji
kujiboresha safu ya ulinzi licha ya kumaliza katikati ya msimamo wa ligi msimu
uliopita na ilikuwa timu iliyofungwa mabao mengi zaidi. Pengine hii ndio sababu
ya Makelele aliyekuwa na sifa ya kulinda kupewa timu.
Mchezaji
mkongwe, Mickael Landreau-aliyecheza timu ya Taifa na Makelele-amestaafu na
sasa Bastia wamemchukua kwa mkopo Alphonse Areola kutoka PSG, huyu ni kipa wa
Ufaransa wa timu ya vijana chini ya miaka 21.
Makelele
ana uzoefu mkubwa wa aina ya wachezaji anaotaka kufanya nao kazi. Beki wa kati
wa zamani wa Asernal, Sebastien Squillaci amevutia kurudi Ligue 1, kiungo wa
Ivory Coast, Romaric na Djibril Cisse wanabaki kuwa wachezaji muhimu.
Pia
kuna wachezaji wengine muhimu kama vile Francois Modesto na Mbelgiji
aliyesajiliwa kwa mkopo, Guillaume
Gillet wanaweza kuwa msaada mkubwa kwake.
Mchezaji
kiongozi uwanjani, mtu anayefanya kazi ya Makelele, Yannick Cahuzac ataimarisha
safu ya ulinzi na kwa vile alizaliwa Corsica na kucheza Bastia maisha yake yote
ya soka, bila shaka atapata nafasi ya kuwa nahodha.
Makelele
atakuwa mvuto mkubwa msimu ujao.
WILLY
SAGNOL, BORDEAUX
Huyu
ni mchezaji mwingine wa kimataifa wa zamani wa Ufaransa ambaye amepewa jukumu
la kuinoa klabu ya Ligue 1.
Sagnol
alikuwa chaguo la pili la Bordeaux, chaguo la kwanza lilikuwa Zinedine
Zidane aliyeichezea klabu hiyo kwa miaka
minne katikati ya miaka ya 1990.
Aliamua
kuendelea kubakia Real Madrid na Sagnol aliteuliwa badala yake na hii ni baada
ya kuonesha uwezo mkubwa akiwa na timu ya Ufaransa ya vijana chini ya umri wa
miaka 21 na kuipiga chini kazi ya Lyon.
Kitu
kinachovutia kwa kocha huyu ni kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Alipoulizwa swali kuhusu mchezaji mtukutu, Joey Barton, hakujibu kwa woga.
“Barton,
ndiyo, ni mjinga. Hajawahi kushinda chochote, maisha yake ya soka yamejaa
matatizo,” Sagnol alijibu mapigo.
Wakati
huo huo, havutiwi na maoni ya waandishi wa habari kuhusu timu yake.
“Kwangu
mimi, mwandishi hana ufundi inapokuja kwenye suala la mpira, na kocha hajui
lolote kuhusu uandishi wa habari,” anasema. “Mara zote naongea na marafiki
zangu waandishi. Halafu wanasema, “Tumekuwa tukitazama mechi kwa miaka 20.’
Lakini nimekuwa nikitizama filamu kwa miaka 20, lakini sijawahi kufikia hatua
ya kukosoa hata kipande kimoja cha Sinema.”
Baada
ya kumaliza nafasi ya 7 msimu uliopita, Sagnol anatarajiwa kumaliza katika
nafasi nne za juu.
Magoli
yanaweza kutoka kwa mshambuliaji hatari Cheick Diabate, ingawa kuondoka kwa nyota
wake, Ludovic Obraniak aliyejiunga na Werder Bremen ni pengo kubwa. Kwasasa
Gregory Sertic, kijana mwenye kipaji cha juu ndiye mchezaji mpishi pekee
aliyesalia klabuni.
PIPPO
INZAGHI, AC MILAN
Miongoni
mwa magwiji wa Milan ambao ni pamoja na Alessandro Nesta, Paolo Maldini, Rui
Costa na wengineo, hakika usingemfikiria Inzaghi kama ataingia kwenye mambo ya
utawala.
Lakini
baada ya kuona nusu msimu wa shujaa mwingine wa Milan Clarence Seedorf na
kutimuliwa kazi, Inzaghi anarithi mikoba yake kutoka timu ya vijana ya timu hiyo.
Kurudi
kwa Jeremey Menez kumeongoza makali safu ya ushambuliaji ya AC Milan. Menez
anaungana na nyota wengine, Stephan El Shaarawy, Mario Balotelli na Keisuke
Honda na sasa amejumuika Hachim Mastour ambaye anatarajiwa kupewa nafasi.
Tatizo
kubwa la AC Milan ni wachezaji kubadilika badilika na kazi kubwa ya Inzaghi ni
kukiunganisha kikosi na kuwapa motisha wachezaji.
Msimu uliopita Milan walimaliza nafasi ya
chini zaidi baada ya kupita miaka 16, sababu si kwamba hawakuwa na wachezaji
wenye vipaji. Kazi imebaki kwa Inzaghi kuhakikisha anajenga heshima kuliko
Seedorf.
Inzaghi
anaonekana kuwa na mfumo wa kumiliki zaidi mpira,pengine sawa sawa na AC Milani
ya katikati ya mwaka 2000. Katika mazoezi, amekuwa akisisitiza wachezaji wake
kupiga pasi za haraka kwenda mbele ili kushambulia zaidi.
Je, Inzaghi ataendelewa
kuwepo AC Milan baada ya msimu ujao? Tusubiri.
COSMIN CONTRA, GETAFE
Kazi kubwa ya Cosmin ni
kurudisha nguvu ya Getafe iliyokosa mashabiki wenye mapenzi ya kweli.
Beki huyo za zamani wa
kulia wa Getafe, alicheza miaka minne klabuni hapo.
Gentra alikuwa chaguo la
kwanza. Alikuwa na msimu mzuri kama kocha huko Romania ambapo alifanya kazi
nzuri katika klabu ya Fuenlabrada.
Getafe ni klabu ngeni
ambayo uwanja wake umekosa morali na siku zote unakuwa bila mashabiki. Sababu
kubwa ni ukosefu wa fedha za kununua wachezaji wakubwa. Ni kazi ya kocha
kuwahamasisha wachezaji ili wawe imara kuendana na mazingira halisi.
Hata hivyo, Contra
amemsajili Mfaransa Karim Yoda aliyeonesha kiwango kizuri huko Romania, akiisaidia
timu yake ya Astra Giurgiu kumaliza nafasi ya pili ambayo hawajahi kushika.
Uimara pekee wa Getafe ni
kasi ya washambuliaji wake- kwa mfumo wa Contra, timu hii itakuwa hatari zaidi.
ZINEDINE ZIDANE, REAL
MADRID CASTILLA
Zidane pekee katika orodha
hii, ndiye kocha anayafanya kazi nje ya ligi kubwa.
Lakini kama sehemu ya
kizazi hiki, ni ngumu sana kuridhika na kazi yake ya kuifundisha Real Madrid B.
Lakini inaonekana anaandaliwa kumrithi Carlo Ancelotti katika kazi ya kocha wa
timu ya kwanza.
Kiukweli, Real Madrid
wanamuandaa Zidane kama Barcelona walivyofanya kwa Pep Guardiola.
Kazi kubwa ya Zidane ni
kuendeleza vipaji changa na pengine atamkuza zaidi mtoto wake mwenye miaka 19,
Enzo ambaye anatumia jina la ukoo wa mama yake, Fernandez.
Enzo amepandishwa kutoka
Juvenil A mpaka kikosi cha Castilla kwa ajili ya msimu wa 2014-15, akivaa jezi
namba 10 aliyokuwa anavaa Zidane akiwa na timu ya Real Madrid na Ufaransa na
amekuwa akicheza kama baba yake, hususani kumiliki mpira na kupiga krosi.
Pia watoto watatu wa
Zidane,--Luca miaka 16, Theo (12) na Elyaz (8) wapo katika akademi ya Real
Madrid, hivyo atafanya nao kazi.
Lakini nani anajua? Muongo mmoja
ujao, Zidane anaweza kuwa kocha wa timu ya wakubwa ya Real Madrid akiwa na
watoto wake wanne kwenye kikosi.
0 comments:
Post a Comment