Imechapishwa Agosti 1, 2014, saa 4:02 asubuhi
JOSE Mourinho ameweka wazi kuwa kipa namba moja wa
muda mrefu wa Chelsea, Petr Cech anaweza kuondoka klabuni hapo majira haya ya
kiangazi mwaka huu.
Baada ya Thibaut Courtois kurejea klabuni kutokea
klabu ya Atletico Madrid alipokuwa anacheza kwa mkopo, tetesi zimeshaanza
kuzuka kama kipa wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech ataendelea kushikilia namba
moja katika dimba la Stamford Bridge.
Mtandao wa Goal
unafahamu kuwa Chelsea wapo tayari kusikiliza ofa kutoka klabu ya PSG
iliyoonesha nia , na Mourinho amesema Cech anaweza kuondoka kwa kutegemea Mark
Schwarzer kuwa kipa namba mbili.
“Petr yupo tayari kupigania nafasi yake, lakini
Thibaut ni kipa bora zaidi kijana duniani, hakuna wasiwasi juu ya hilo,” Kocha
huyo Mreno alikaririwa akizungumza na Evening
Standard.
“Watachuana na kwangu mimi ni tatizo zuri la
kufanya maamuzi.
“Sisi ti timu inayohitaji kuwa imara na
kushindania makombe na tunahitaji ushindani wa nafasi.
Courtois amerudi klabuni baada ya kuonesha kiwango
kizuri akiwa na timu ya taifa ya Ubelgiji na amesisitiza kuwa anahitaji
kutengeneza jina nchini England kama alivyofanya Hispania.
“Nilisaini mkataba hapa miaka mitatu iliyopita,
kwasasa nina furaha ya kuwa hapa, kuwa sehemu ya klabu,” aliiambia Tovu rasmi
ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment