
Aliachwa: Angel Di Maria hakupangwa katika kikosi cha Real Madrid kilichokabiliana na Atletico Madrid jana usiku.
CARLO Ancelotti amethibitisha kuwa mchezaji anayewaniwa kwa nguvu zote na Manchester United, Angel Di Maria aliachwa katika kikosi cha jana kwenye mchezo wa marudiano wa Spanish Super Cup dhidi ya mahasimu wake, Atletico Madrid na kupoteza kombe la kwanza msimu huu kwa sababu za kimpira na si vinginevyo.
"Aliachwa katika kikosi kwa sababu za kimpira" Alisema Ancelotti alipoulizwa kwanini hajampanga Muargentina huyo hata katika orodha ya wachezaji wa akiba jana uwanja wa Vicente Calderon.
Kitendo cha Di Maria kutopangwa jana kinaashiria uhusiano na kocha Ancelotti umefikia hali mbaya na ni sababu tosha kwa Manchester United kumnasa kwa ada inayoaminika kuwa paundi milioni 50.
Ancelotti alithibitisha kuwa nyota huyo wa Argentina katika fainali za kombe la Dunia majira ya kiangazi mwaka huu ameomba kuondoka Real Madrid.

Mashabiki wa Real Madrid wameiacha klabu katika wasiwasi kwasababu wanamhitaji Di Maria kubakia, lakini Rais Florentino Perez anataka auzwe ili kuweka sawa mahesabu baada ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili Toni Kroos na James Rodrgiguez.
Madrid walibaki katika utata mkubwa kutokana na mashabiki waliohudhuria Santiago Bernabeu siku ya jumanne kulipuka kwa shangwe wakimshangilia Di Maria baada ya kuingia uwanjani kipindi cha pili akitokea benchi.
Ancelotti alithibitisha ijumaa kuwa mchezaji amekataa kusaini mkataba mpya na ameomba kuondoka.
0 comments:
Post a Comment