Imechapishwa Julai 30, 2014, saa 3:31 asubuhi
KIUNGO wa mabingwa wa England, Manchester City,
Yaya Toure amesema anataka kubakia klabuni hapo kwa muda mrefu kadiri
itakavyowezekana.
Nyota huyo mwenye miaka 31 mapema mwaka huu
aliripotiwa kutimka Etihad baada ya wakala wake, Dimitri Seluk kusema kuwa
Toure alijisikia kutothaminiwa na klabu baada ya kutotumiwa salamu za siku ya
kuzaliwa mwezi mei.
Toure mwenye alieleza kuwa anavutiwa kujiunga na matajiri
wa Ufaransa, Paris Saint-Germain.
Siku za nyuma Toure alisema kwamba, mashabiki
wasisikilize maneno ambayo hayajatoka mdomoni mwake, lakini kila asemacho
Dimitri ni sahihi kwasababu anazungumza kwa niaba yake, ingawa kwasasa
anasisitiza kuwa wakati wote amekuwa kimya kuhusu furaha yake na hatima yake ya
baadaye.
Muivory coast huyo aliiambia tovuti ya klabu kuwa
ana nia ya kuendelea kubakia Man City, na aliongeza kuwa ameweza kukabiliana
vizuri na tetesi za yeye kuondoka Etihad.
Toure alieleza: “Halikuwa jambo la kuondoka klabuni,
ni ngumu sana kwasababu mazingira yangu ni magumu. Tunapotakiwa kufanya kitu fulani,
tulitakiwa kutoa maelezo. Kwangu mimi ni kawaida…mara zote nilikuwa kimya”.
“Na mwisho wa siku ni maamuzi yangu. Kama unaseme
kwamba, nitasema kwamba. Kama hupendi hilo, nitasema tena hilo na kama unapenda
hilo, nitasema, kwangu mimi ni jambo sahihi, na nitakaa Man City kwa muda mrefu
kadiri iwezekanavyo”.
Toure alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha
Manuel Pellegrini kilichotwaa ubingwa akifunga mabao 20 katika michezo 35
aliyocheza msimu uliopita, lakini amesisitiza kuwa City lazima ijipange
kuelekea msimu wa 2014/2015 kwasababu ya vipaji vinavyoendelea kufurika katika
klabu za ligi kuu.
“Kwasasa nina furaha ya kujiunga na timu na kocha
kwasababu ni kocha wa ajabu,” Alisifu. “Kila mtu ana furaha. Mwaka uliopita
ulikuwa msimu mzuri”.
“Mwaka huu utawakuwa wa kushangaza kwasababu timu
zote kubwa zinasajili wachezaji wazuri. Kwa upande wangu, jambo la kwanza ni
kurudi kwa nguvu tena”.
Toure alikiri kuwa miezi michache iliyopita, yeye
na familia yake walikuwa katika hali ya huzuni kufuatia kufariki kwa kaka yake,
Ibrahim baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.
“Najisikia vizuri,” alisema kiungo huyo. “Ni
vizuri nimeanza mazoezi tena. Kwa bahati mbaya wakati wa mapumziko ulikuwa mgumu
kwa familia yangu”.
0 comments:
Post a Comment