Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 1:52 usiku
BAADA ya kuenea kwa taarifa jioni ya
leo kuwa Yanga sc imejitoa kushiriki michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki
na kati maarufu kama Kombe la Kagame, uongozi wa Yanga umekanusha taarifa hizo.
Ilielezwa kuwa Yanga wameamua
kujitoa katika michuano hiyo inayoanza kushika kasi Agosti 8 mwaka huu Mjini
Kigali nchini Rwanda kwasababu kikosi chao hakijapata barua rasmi ya mwaliko.
Lakini ilisemekana kocha mkuu wa
Yanga, Mbrazil , Marcio Maximo ameamua kujitoa kombe la Kagame kwasababu kikosi
chake hakipo tayari kushiriki michuano yoyote ndani ya wiki mbili zijazo.
Kutokana na nusu ya wachezaji wa kikosi
cha kwanza kuwepo katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania iliyoanza jioni ya
leo mjini Tukuyu mkoani Mbeya, kocha Maximo ameona bora kujitoa.
Hata hivyo baada ya taarifa hizo,
Yanga kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa facebook imesema
kwamba haijajitoa kushiriki mashindano ya Kombe la Kagame chini Rwanda kama
inavyoripotiwa na baadhi ya mitandao ya habari nchini na kusema taarifa hizo ni
za uongo.
Katibu mkuu wa Yanga SC
Bw Beno Njovu amesema taarifa hizo zilizosambazwa ni za uongo na kuwa kwa siku
ya leo hajaongea na mwandishi wa habari yoyote juu ya michuano hiyo.
“Sie hatujatangaza
kutoshiriki michuano ya Kagame, kama tulivyosema awali kikubwa tunasubiri
taarifa rasmi za kushiriki kutoka CECAFA
0 comments:
Post a Comment