WAYNE
Rooney anahitaji kuwa nahodha wa Manchester United kuelekea kusaka ubingwa,
lakini amesisitiza kuwa ataheshimu maamuzi ya kocha mkuu Louis Van Gaal kwa
yeyote atakayemchagua.
Robin
Van Persie anatajwa kuchaguliwa kuwa
nahodha wa United kutokana na mahusiano mazuri aliyonayo na kocha Van Gaal
kuanzia timu ya taifa ya Uholanzi.
Wakati
huo huo Darren Fletcher alivaa kitambaa cha unanodha katika ushindi wa 7-0
dhidi ya La Galaxy alhamisi ya wiki hii.
Rooney
ana imani kuwa Man United itafuta makosa ya msimu uliopita chini ya kocha Van
Gaal ambapo ilimaliza katika nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu soka nchini
England.
“Kiukweli
tunaweza kushinda ubingwa,” aliwaambia waandishi wa habari. “Msimu uliopita
tulikuwa wabaya sana, tunajua hilo, lakini tuna imani tutafanya vizuri.
Tunatakiwa kuamini kuwa tunaweza kutwaa ubingwa”.
“Sio
siri, ningetamani kuwa nahodha, lakini ni maamuzi ya kocha kuchagua anayemtaka.
Anahitaji kufanya kazi na wachezaji na kuchagua nahodha kutoka kwa wachezaji
hao”.
“Sidhani
kama anaweza kutoka nje na kuchagua nahodha. Nina uhakika atachagua miongoni
mwa wachezaji walioopo na kufikia maamuzi wiki zijazo”
0 comments:
Post a Comment