Kuanzia kushoto, Luis Figo, Zinedine Zidane na Ronaldo de Lima
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 22, 2014, saa 11:26 jioni
VODACOMA Tanzania ni miongoni mwa makampuni
yaliyojitokeza kudhamini ziara ya magwiji waliocheza kwa
mafanikio makubwa katika klabu ya Real Madrid.
Kikosi cha magwiji hao maarufu kama `Real
Madrid Legends` kitafanya ziara ya siku nne nchini kuanzia Agosti 22 mwaka huu
na kitacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya kikosi maalumu cha nyota wa
Tanzania.
Akizungumza leo na waandishi wa habari
katika hoteli ya New Afrika, jijini Dar es salaam, meneja
wa ziara hiyo, Dennis Ssebo amesema mbali
na Vodacom, wadhamini wengine ni Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM
Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
Ziara hiyo ni mwaliko wa kampuni ya
Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya mkurugenzi wake mkuu, Farough
Baghozah na meneja wa ziara hiyo ni Dennis Ssebo.
Wachezaji wa Real Madrid waliocheza La
Liga miaka ya nyuma, ligi ya mabingwa kombe la dunia kama vile Mfaransa
Zinedine Zidane, Mreno Luis Madeila Figo na Mbrazil Ronaldo de Lima watakuwepo
katika ziara hiyo.
Ssebo kabla ya mkutano wa leo,
aliuambia mtandao huu kuwa maandalizi ya ziara hiyo yanakwenda vizuri na
itakuwa fursa pekee kwa Watanzania kuiona Real Madrid kwa mara ya kwanza barani
Afrika.
“Ninaloweza
Kusema ni kwamba, Watanzania wakae tayari kupokea wachezaji 27 wa zamani
wa timu ya Real Madrid na mashabiki 23 kutoka Hispania wanaokuja
kuwashangilia magwiji wao. Kwahiyo jumla tunapokea watu 50 kutoka Hispania kwa
ajili ya ziara hii”. Alisema Ssebo.
“Ni ziara ambayo tulifikiria itakuwa
fupi, lakini wenzetu kumbe wameipenda nchi na wanaifahamu, kwahiyo ni ziara
ambayo itachukua takribani siku nne”. Aliongeza.
0 comments:
Post a Comment