Imechapishwa Julai 24, 2014, saa 1:18 asubuhi
MOJA ya stori kubwa kwasasa nchini
Tanzania ni ujio wa kikosi cha magwiji wa Real Madrid maarufu kama `Real Madrid
Legends`.
Wanandinga hao wa zamani waliotamba na
Real Madrid kwenye michuano ya La Liga , UEFA pamoja na kombe la dunia wakiwa
na nchi zao watafanya ziara ya siku nne
nchini kuanzia Agosti 22 mwaka huu na kitacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya
kikosi maalumu cha nyota wa Tanzania.
Meneja wa ziara
hiyo, Dennis Ssebo alibainisha kuwa Vodacom Tanzania ni miongoni mwa wadhanimi
wa ziara hiyo. Wadhamini wengine ni Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas,
EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
Ziara hii ni mwaliko wa kampuni ya
Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya mkurugenzi wake mkuu, Farough
Baghozah na meneja wa ziara hiyo ni Dennis Ssebo.
Moja ya mjadala unaoendelea kwa sasa
ni pamoja na kujua faida ya ujio wa wachezaji hawa wa zamani, waliotamba na
kutikisa ulimwengu wa soka kwa ngazi ya klabu na kimataifa.
Kiuhalisia kabisa, Kuja kwao nchini kuna faida au
fursa nyingi nje ya ujio huo. Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii na
bodi ya utalii wanatakiwa kuichangamkia hii tenda na kuwa sehemu ya udhamini sanjari
na makampuni yanayowezesha ziara hiyo ya akina Luis Figo, Zinedine Zidane,
Fabio Cannavaro, Ronaldo De Lima na wengineo.
Kiukweli hili ni bonge moja la fursa kwa
makampuni, serikali kupitia bodi ya utalii kuwa sehemu ya udhamini ili
kujitangaza kitaifa na kimataifa.
Kwa bahati mbaya sana, Tanzania hatujui mahala pa
kuweka hela, watu wengi ambao wapo kwenye maeneo mengi, si sahihi kwa maana kwamba
wamekosa ueledi wa kung`amua fursa kwa haraka na kuwekeza ili ‘kupiga mtonyo’
wa ukweli.
Utashangaa
kuona ujio wa timu kama ile unachukuliwa poa tu, wanapotezewa watu kama Figo,
mwanasoka bora wa Ulaya, watu kama Zidane aliyetwaa kombe la dunia na UEFA, mwanasoka
bora wa ulaya na duniani kote.
kumbe ingekuwa nchi nyingine, hii ni fursa ya
kujitangazwa kwasababu atakachokifanya Figo, Zidane au Cannavaro, vyombo vya
habari ulimwenguni kote vinafuatilia hiyo stori.
Kwahiyo wakienda kama Mlima Kilimanjaro na sehemu
nyingine ya vivutio vya utalii, ni fursa moja rahisi sana kuitangaza nchi
kupitia kwa wale jamaa.
Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatakiwa
kutumia fursa hii kujitangaza kimataifa na kitaifa. Ndio maana unaona nchi
nyingine zinawatumia wachezaji hao kama mabalozi.
Kwanini wanawatumia kama mabalozi? kwasababu watu wale
ni maarufu tayari na wana watu wengi nyuma yao (mashabiki).
Zinedine Zidane atakuwepo nchini mwezi ujao
Kama kuna fursa ya wao kuja, watumike zaidi ya
kuenda uwanja wa taifa kucheza mpira na kuwashuhudia ‘Laivu’, halafu kupiga picha
tu.
Ujio wao uwe na tija, makampuni mengi ya simu,
benki na mengineyo, yanatakiwa kujihusisha na wale watu na itakuwa rahisi kuwafikia wateja.
Kwa mfano Luis Figo akipiga picha mbele ya bango
la Vodacom au Tigo kwa maana ya wao kuwa wadhamini na ‘akipostiwa’ kwenye mtandao
wa kijamii wa Instagram au facebook, gazeti, TV au sehemu yoyote ile, watu
wangapi wataiangalia.
Watu wangapi watapenda kuona mahojiano ya Figo,
halafu huku nyuma kuna nembo ya kampuni yoyote ile? Ni wengi sana.
Kwahiyo kuna fursa ya serikali kupitia taasisi
husika na makampuni kujitangaza kupitia ujio wa hawa wachezaji na kujinufaisha
kuliko kuwachukuliwa poa tu.
Mkurugenzi wa bodi ya Utalii Tanzania Balozi Charles
Sanga na meneja wa masoko wa bodi hiyo, Geofrey Meena wanatakiwa kuufikiria
mara mbili ujio wa wachezaji hawa na kutumia fursa hiyo kujitangaza kimataifa.
Chanzo: Shaffihdauda.com
0 comments:
Post a Comment